shilingi 5,200,000,000 zinatarajiwa kulipwa kwa wananchi


Jumla ya shilingi 5,200,000,000 zinatarajiwa kulipwa kwa wananchi wa mitaa ya Likong'o na Mtikavu, manispaa ya Lindi ambao wataacha maeneo yao kupisha ujenzi wa mradi wa kusindika gesi asilia(LNG).

Hayo yalielezwa jana mjini Lindi, na mkurugenzi   mkuu wa shirika la maendeleo ya petroli(TPDC), Dkt James Mataragio alipozungumza na waandishi wa habari.

Dkt Mataragio alisema walikwenda ofisini kwa mkuu wa Lindi, Godfrey Zambi ili kumtaarifu utaratibu utakaotumika kuwalipa wananchi hao ambao wataachia maeneo yao ya ardhi ili kupisha ujenzi wa mradi huo.

Alisema tangu serikali kupitia TPDC ichukue maeneo hayo mwaka 2015, juhudi za kutafuta fedha kwa ajili ya kuwalipa fedha, ikiwa ni fidia ya maeneo yao wananchi waliyoachia kwa ajili ya ujenzi huo.

Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba zoezi la kuwalipa wananchi hao ambao idadi yao ni 653 litaanza tarehe 9 na kumalizika tarehe 17, mwezi Mei, mwaka huu. Ambapo  litatanguliwa na utoaji elimu kwa wananchi hao, ikiwamo jinsi ya kufungua akaunti za benki.

'' Kumekuwa na taarifa zisizo za kweli kuhusu mradi huu. Sasa kitendo cha serikali kutoa fedha hizo
ni ushahidi kwamba serikali imejizatiti kutekeleza mradi huu,'' alisema Dkt Mataragio.

Kwa upande wake, mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi aliwataka wananchi wanaotarajia kulipwa fidia wafungue akaunti benki, kwani hakuna atakayelipwa fedha mkononi.

Nakwamba halmashauri ya manispaa ya Lindi itawagawia viwanja na hati za kumiliki viwanja hivyo.

Post a Comment

0 Comments