tangazo

Boss Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) akagua vichwa saba vya treni katika Karakana ya Reli Morogoro


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusidedit Kakoko ametembelea Karakana ya Reli iliyopo mkoani Morogoro kwa lengo la kukagua matengenezo ya vichwa saba vya treni.

Vichwa hivyo vya treni ndivyo vitakavyosaidia usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam hadi Bandari Kavu ya Kwala-Ruvu pamoja na Yadi ya Ubungo.

Akiwa katika Karakana hiyo leo Mei 8 mwaka huu,Mkurugenzi huyo wa TPA ameelezwa na wataalam wa Karakana hiyo kuwa vichwa vinne vitakamilika mwishoni mwa Juni 2020 na vilivyosalia vitakamilika mwezi Agosti 2020.

Mkurugenzi Mkuu ameridhishwa na kazi hiyo na amewapongeza wataalam hao kwa kazi nzuri na kujituma."

Hata hivyo wakati utengenezaji wa vichwa hivyo ukiendelea katika karakana hiyo kwa ajili ya usafirishaji mizigo kutoka Dar es Salaam hadi Bandari ya Kwala, tayari makontena 49 yameshawasili katika Bandari Kavu ya Kwala.

 Wataalam walioko kwenye Karakana ya Reli iliyopo mkoani Morogoro wakiwa makini kumsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Deusidedit Kakoko alipotembelea karakana hiyo kuangalia matengenezo ya vichwa saba vya treni

Post a Comment

0 Comments