tangazo

Diamond kuja na tamasha la Wasafi Quarantine festival

Mmiliki wa lebo ya muziki ya wcb_wasafi, Diamond Platnumz ni mfanyabiashara ambaye anatumia kila fursa inayopita mbele yake bila ya kuogopa chochote.

Msanii huyo ametangaza ujio wa tamasha la "Wasafi Quarantine Festival" ambalo litafanyika mwaka huu. Ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Taarifa ya ujio wa Tamasha hilo limetoka siku chache baada ya WCB kuachia ngoma yao ya pamoja iitwayo "Quarantine" ambapo Rayvanny, Mbosso_ Lavalava wamehusika huku mwanadada Zuchu akiwashangaza maelfu ya mashabiki zake kwa namna alivyobadili namna ya uimbaji wake.

Aidha, kwenye taarifa yake ya awali aliyoitoa usiku huu, bosi wa Lebo hiyo, msanii Diamond Platnumz bado hajabainisha ni lini tamasha hilo litaanza kufanyika.

Post a Comment

0 Comments