Mpaka Sasa Hakuna Mbunge aliyeripoti ofisi ya mpelelezi - Kamanda Mambosasa

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema kuwa mpaka sasa hivi hakuna Mbunge yeyote aliyeripoti kwenye ofisi ya Mpelelezi wa kanda hiyo, kutokana na kukiuka kwa agizo la Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda, aliyewapa masaa 24 kurudi Bungeni.

Kamanda Mambosasa ameyabainisha hayo leo Mei 9, 2020, alipoulizwa kama kuna Mbunge yeyote aliyeripoti kwa hiyari yake kama ambavyo Jeshi la Polisi lilivyoagiza siku ya Mei 7.

"Hakuna hata mmoja aliyeripoti, inawezekana hawapo Dar es Salaam na ndiyo maana nilisema kama kuna yeyote bado yupo, na hakuna aliyepatikana pia, hatujawasaka lakini ule ulikuwa ni wito" amesema Kamanda Mambosasa.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alitoa masaa 24 kwa Wabunge ambao wako Jijini humo, waondoke na kurejea Dodoma kuendelea na shughuli zao za Bunge na atakayekaidi basi atakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa nyakati za usiku.

Post a Comment

0 Comments