tangazo

Saudi Arabia yapandisha kodi ya bidhaa muhimu mara tatu


Saudi Arabia imetangaza leo kupandisha mara tatu kodi katika bidhaa muhimu, ambazo zimepanda hadi asilimia 15 na kupunguza matumizi katika miradi mikubwa kwa kiasi cha dola bilioni 26 wakati ikikabiliana na athari za janga la virusi vya corona pamoja na bei ya chini ya mafuta katika uchumi wake.

Wananchi wa Saudia pia watapoteza fedha za marupurupu ya gharama za maisha ambazo zimekuwa zikitolewa tangu mwaka 2018, kwa mujibu wa waziri wa fedha wa nchi hiyo. Licha ya juhudi za kutafuta vyanzo vingine katika uchumi wa nchi hiyo, taifa hilo la kifalme linaendelea kutegemea kwa kiasi kikubwa mapato ya mauzo ya mafuta.

Bei ya mafuta hivi sasa inafikia dola 30 kwa pipa, ikiwa ni chini ya kiwango ambacho Saudi Arbia inahitaji kuweka uwiano katika bajeti yake.

Taifa hilo pia limepoteza fedha kutokana na kuzuiwa kwa muda hija katika miji mitakatifu ya Mecca na Medina, ambayo imefungwa kutokana na janga la virusi vya corona.

ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments