Musa Faki Muhammed , kiongozi wa Umoja wa Afrika ametolea wito Marekani kuondoa kila jambo ambalo linaviashiria vya ubaguzi.
Umoja wa Afrika kupitia kiongozi wake Musa Faki Muhammed umetoa wito kwa Marekani kuingilia kati na kuondoa viashiro vyote ambavyo vinaonekana kuwa ni vitendo vya kibaguzi nchini Marekani.
Katika taarifa yake ya maandish, Muhammed Musa Faki amekemea ghasia na ukiukwaji wa haki wa maafisa wa jeshi la Polisi Minneapolis na kitendo kilichopelekea kuuawa kwa mmarekani mweusi .
Musa Faki ametoa salamu za rambi rambi kwa familia ya George Floyd, mmarekani aliuawa kwa kukandamizwa na goti shingoni na askari ambae bila shaka hakuwa na roho ya kibinadamu.
Kiongozi huyo wa Umoja wa Afrika amekumbusha kuwa wakati wa kuanzishwa Umoja wa huo, ulikuwa ukikemea matendo ya kibaguzi tangu mwaka 1964 .
Musa Faki ameendelea akisema kwamba viongozi nchini Marekani wanatakiwa kuongeza juhudi zao katika jitihada za kuzingatia usawa na kuebuka aina yeyote ya ubaguzi wa rangi.
Umoja wa Afrika umekemea vikali matendo ya kibaguzi dhidi ya mtu mweusi nchini Marekani.
0 Comments