tangazo

Virusi vya corona: Fahamu kinachotokea ndani ya mwili mtu akipata virusi hivi

Virusi vya corona vilitokea Desemba mwaka jana lakini tayari dunia nzima inakabiliana na janga hili la Covid-19.

Kwa wengi ugonjwa huu unajitokeza nguvu yake ikiwa ya wastani tu lakini baadhi ya watu hufa.

Lakini je virusi hivi vinaathiri vipi mwili, kwanini baadhi ya watu wanakufa na je tiba yake ikoje?

Muda wa kuatamia wa kirusi cha Corona

Hiki ni kipindi ambacho kirusi kinajiimarisha kwenye mwili.

Kirusi huingia kwenye seli zinazotengeneza mwili na kuziteka nyara.

Coronavirus, inayojulikana pia kama Sars-CoV-2, inaweza kuvamia kwenye mwili unapopumua yaani baada ya mtu mwenye virusi kukohoa ama kushika sehemu yenye virusi hivyo na kushika uso wako.

Kwanza inaambukiza seli za kwenye koo lako, njia za kupumua na kwenye mapafu na kuzibadilisha kuwa sehemu ya utengenezaji wa virusi vya corona, na kuzalisha virusi vingi vipya ambavyo vinaenda kuathiri seli nyingi zaidi.

Katika hatua hii, bado utakuwa hujaanza kuumwa na kuna baadhi ya watu ambao hata hawaoneshi dalili zozote kabisa.

Kipindi hiki cha kirusi kutamia, muda kati ya mambukizi na dalili ya kwanza kujitokeza, inatofautiana kabisa lakini kwa wastani ni siku tano.

Mlipuko wa virusi vya Corona unasambaa kwa

Nguvu ya Corona inapokuwa ya wastani mwilini

Idadi kubwa ya watu inapitia kiwango hiki cha virusi vya corona

Covid-19 ni maambukizi kwa watu kati ya wanane na kumi na dalili zake zinakuwa sio kali sana na dalili kubwa ni joto na kukohoa.

Mwili unauma, koo linawasha na kichwa kuuma vyote vinawezekana lakini sio lazima dalili hizo kujitokeza kwa namna hii.

Kuwa na joto na kujihisi vibaya tu kwa ujumla ni kwasababu mfumo wa kinga unapigana na maambukizi hayo.

Hii ina maanisha kwamba mwili umetambua umevamiwa na virusi na ni dalili kwamba kuna kitu ambacho hakiko sawa mwilini mwako kwa kutoa dutu za sitokini yaani cytokines kwa kiingereza kutoka kwenye baadhi ya seli za mfumo wa kinga ambazo zinathiri seli nyengine.

Zinafanya mfumo wa kinga kuendelea kurejea katika hali yake ya kawaida lakini pia zinafanya mwili kuuma, kupata maumivi na homa.

Kikohozi cha coronvirus mara ya kwanza huwa ni kikavu na pengine hili ni kwasababu ya seli zinazowasha baada ya kupata virusi.

Baadhi ya watu hatimaye wataanza kutoa makohozi yenye seli zilizouliwa na virusi kwenye mapafu.

Dalili zake zinatibika kwa mtu kupumzika vizuri, kunywa maji mengi na kupata dawa za maumivi. Huhitaji kupata matibabu maalum hospitalini.

Hatua hii itadumu kwa takribani wiki moja - hatua ambayo wengi hupata afueni kwasababu mfumo wa kinga umekabiliana na kirusi.

Hata hivyo baada ya hatu hiyo, baadhi ya watu hali zao huzorota zaidi na kuonesha dalili kali za kirusi hiki cha Covid 19.

Hadi kufikia sasa, hiki ndicho kinachofahamika kutokea katika hatua hii, ingawa kuna baadhi ya tafiti zinazoonesha kwamba ugonjwa huo unaweza kusababisha dalili za homa zaidi kama vile kuwa na mafua pia.

Kinachotokea mwilini mtu akiwa katika hali mbaya zaidi

Ikiwa ugonjwa huu utaendelea hilo litakuwa ni kwasababu ya mfumo wa kinga kutumia nguvu nyingi katika kukabiliana na kirusi cha corona.

Kemikali zinazotolewa mwilini zinasababisha uvimbe, na hili pia inategemea na kiwango cha athari. Uvimbe mkumbwa unaweza kusababisha uharibifu mkubwa kwenye mwili.

"Kirusi hiki kinasababisha ukosefu wa uwiano wakati mfumo wa kinga unakabiliana na kirusi, kunakuwa na uvimbe kwa kiasi kikubwa lakini vile hili linavyotendeka bado haijafahamika," amesema Dr Nathalie MacDermott, kutoka chuo cha King College London.

Lungs infected with coronavirusHaki miliki ya pichaSPL
Image captionMapafu yaliyoathirika na virusi vya corona na kuonesha sehemu zenye nimonia

Kufura kwa mapafu kunafahamika kama nimonia

Iwapo ingewezekana mtu kusafiri kupitia kwenye mdomo basi angefika kwenye mapafu na hatimaye kuishia kuwa kwenye vifuko vidogo vya hewa.

Hapo ndipo oksijeni inakwenda hadi kwenye damu huku hewa chafu ya kaboni dioksidi ikitoka nje lakini kwa nimonia vifuko vidogo vya hewa vinaanza kujaza maji na hatimaye vinafanya mtu kuwa na matatizo au kushindwa kupumua kabisa.

Baadhi ya watu huitaji mashine za kuingiza hewa safi mwilini kusaidia kupumua.

Hatua hii inasemekana huathiri asimilia 14 ya watu kulingana na data kutoka Uchina.

Ugonjwa wa Corona unapokuwa katika hali ya hatari

Inakadiriwa kuwa asilimia 6 ya visa vya ugonjwa huu huwa katika hali mbaya zaidi.

Hadi kufikia hatua hii, mwili unaanza kushindwa kukabiliana na kirusi cha Corona na kuongeza uwezekano wa mtu kifo.

Mfumo wa kinga ya mwili kwa sasa unaanza kushindwa kufanyakazi na kusababisha madhara mwilini.

Pia unaweza kusababisha mshtuko wa moyo wakati shinikizo la damu linaposhuka hadi kiwango cha chini kabisa na viungo kuacha kufanyakazi inavyotakikana na hatimaye kushindwa kabisa.

Hapa unakuwa na matatizo makubwa ya kupumua yanayosababishwa na kufura kwa mapafu na kufanya mwili kukosa hewa safi ya oksijeni inayohitaji ili uweze kupumua. Hali hii inaweza kufanya figo kuacha kufanya kazi kuanzia usafishaji wa damu na kudhuru utando wa utumbo.

"Kirusi hicho kitakuwa kimesababisha kiwango kikubwa cha uvimbe na muda wowote unaweza kufa ... kwasababu viungo vingi sasa vitakuwa vinashindwa kufanya kazi," Daktari Bharat Pankhania amesema.

Na ikiwa mfumo wa kinga utashindwa kuwa imara wakati wa kukabiliana na virusi, hatimaye virusi vitasambaa katika kila sehemu ya mwili na kusababisha madhara makubwa.

ECMO machineHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMgonjwa akitibiwa kwa kutumia mashine ya ECMO inayoingiza oksijeni kwenye damu na kwenda maeneo mengine ya mwili kama vile moyo.

Tiba katika hatua hii, virusi vitakuwa vya kiwango cha juu sana na huenda ukahitaji kutibiwa kwa kutumia mashine ya kusukuma damu hadi maeneo mengine ya mwii kama moyo ya ECMO.

Hii ni njia mbadala inayosukuma damu nje ya mwili wako kupitia mrija mnene na kuingiza hewa ya okisjeni kisha inarejesha tena damu mwilini.

Lakini hatimaye madhara haya yanaweza kusababisha kifo wakati ambapo viungo vitashindwa kabisa kuendesha mwili wako.

Kifo cha kwanza

Madaktari wameelezea vile baadhi ya wagonjwa walivyokufa licha ya kwamba kinga yao ilikuwa inajitahidi kupambana kabisa na virusi hivi.

Wagonjwa wawili wa kwanza waliokufa katika hospitali ya Jinyintan mjini Wuhan, China, kulingana na jarida la kitabibu la Lancet, walikuwa katika hali nzuri ingawa walikuwa wavutaji sigara kwa muda mrefu na hilo likasababisha kudhoofisha mapafu.

Wakati mwanamume wa kwanza, 61, alikuwa anafikishwa hospitalini tayari alikuwa anaugua nimonia.

Alikuwa na matatizo ya kupumua na licha ya kwamba aliwekwa kwenye mashine ya kusaidia kuingiza hewa safi, mapafu yake yalishindwa kufanya kazi na moyo wake ukaacha kupiga.

Mwanamume huyo aliaga dunia siku ya 11 tangu alipofikishwa hospitali.

Mgonjwa wa pili, 69, mwanamume pia naye alikuwa na matatizo ya kupumua.

Aliingizwa kwenye mashine ya kusaidia kusukuma damu ya ECMO lakini hili halikusaidia.

Alikufa kwasababu ya nimonia na alipata mshtuko wa moyo shinikizo lake la damu lililposhuka zaidi.

Post a Comment

0 Comments