Ashikiliwa na polisi kwa kumuua baba yake kwa kumpiga ngumi

KIJANA mmoja Yohana Lameck (17) mkazi wa Wilayani Gairo anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi Issaya Lameck (47) kwa kumpiga ngumi na kumkanyaga sehemu mbalimbali za mwili wake kutokana na ugomvi baina yao.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, mauaji hayo yalitokea Mei 31 majira saa 12 asubuhi katika Kitongoji cha Manyani kata ya Mkalama, Tarafa na Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Kamanda Mutafungwa, amesema mtuhumiwa huyo anaendelea ushikiliwa na polisi na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Wakati huo huo Nuru Hassan (35) mkulima na mkazi wa Kasiki Wilayani Kilosa mkoani hapa anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kupatikana na nyara za Serikali.
Kamanda Mutafungwa, amesema tukio hilo lilitokea Juni Mosi majira ya Saa 1 asubuhi katika kitongoji cha Kasiki ambapo Askari polisi kwa kushirikiana na askari wanyamapori wa hifadhi ya Mikumi wakiwa doria na misako walipokea taarifa za kuwepo kwa mtu mwenye nyara za Serikali na walipofuatilia ndipo walimbaini mwanamke huyo.
Amesema walilazimika kufika nyumbani kwa mwanamke huyo na baada ya upekuzi ndani ya nyumba yake walikuta pembe moja ya ndovu yenye uzito wa kg 7.5yenye thamani y ash 34,635,000.

Post a Comment

0 Comments