tangazo

Watu 14 wameuawa , 90 wajeruhiwa katika shambulizi Marekani

Watu  14  wameripotiwa kuuawa na wengine wasiopungua  90 wamejeruhiwa katika shambulizi la silaha ambalo limetokea katika jimbo la Chicago nchini Marekani.

Shambulizi hilo limeendeshwa na watu ambao bado hawajafahamika.

Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki.

Kuanzia Ijumaa majira ya jiano  hadi Jumatatu asubuhi kuliluwa kikisikika milio ya risasi 104 katika vitongoji tofauti Chicago.

Watu  14 wameripotiwa  kufariki  wakiwemo watoto watano katika mashambulizi hayo.

Tukio hilo ambalo limetokea siku ambayo kukisherekewa siku kuu ya akina baba, watu wasiopungua  90 wameripotiwa kujeruhiwa katika   mashambulizi hayo.

Jeshi la Polisi limefahamisha kwuwa  mtoto mmoja mwenye umri wa miaka  13  alishambuliwa kwa risasi shingoni na kupelekwa hospitali ila  madaktari wakishindwa  kuokoa maisha yake .

Matukio kama yao ya kuvizia  yameendelea katika maeneo tofuati, Polisi imetoa picha za  watu wanaoshukiwa kuendesha mashambulizi hayo na kuendelea kuwasaka.

Post a Comment

0 Comments