DC MKURANGA AWAHIMIZA BODABODA PIKIPIKI KWA MIKOPO NAFUU

 Mkuu wa Wilaya Mkuranga Mhe. Khadija Nassir Ally

DC MKURANGA AFANYA MKUTANO NA MADEREVA BODABODA NA BAJAJI WA WILAYA YA MKURANGA. Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Khadija Nassir Ally amefanya Mkutano na Madereva  wa BODABODA pamoja na bajaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Mkuranga katika uwanja wa Ofisi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.   Katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga amekemea utaratibu unaotumiwa na waendesha boda boda na bajaji kwakubeba abiria zaidi ya idadi inayotakiwa nakuacha kutumia pikipiki kubebea mkaa na baadala yake amewataka kushirikiana na Serikali kwakuomba vibali  kwakushirikiano wao Ili kuweza kubeba mikaa hiyo Kwa vyombo halisi vilivyoruhusiwa kufanya kazi hizo badala ya BODABODA. 

Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka kujiunga pamoja na kuona ni kwanamna gani wanaweza kupata mikopo ya pikipiki na kuzimiliki badala ya kuingia mikataba migumu na makampuni au watu binafsi na kupelekea kukimbia honyo barabarani Kwa lengo la kutimiza malipo ya wamiliki wa vyombo hivyo. 

Kwaupande wao Madereva hao wa BODABODA pamoja na bajaji Wamemshukuru Mkuu wa Wilaya na kumuomba kuwahimiza watu wa Usalama kutumia ustaarabu

kuwakamata BODABODA wanapotaka kukagua makosa pia kuharakishiwa kupata leseni zao Kwa wale waliopata mafunzo.   Mkuu wa Wilaya ameendelea kufanya Mikutano ya makundi mbalimbali ya wananchi Kwa lengo la kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.



Post a Comment

0 Comments