Tetesi za Soka leo



West Ham wameacha nafasi katika kikosi cha wachezaji 25 wa Premier League ambao huenda wakajazwa na mchezaji huru Jesse Lingard.

Lingard, ambaye alivumilia wakati mgumu huko Nottingham Forest kwa muda wa miezi 12 iliyopita, amekuwa akifanya mazoezi na West Ham, baada ya hapo awali alihudumu nusu msimu kwa mkopo mashariki mwa London.

TH

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Tottenham wamemsajili mshambuliaji Zhang Linyan kwa mkopo kutoka klabu ya Ligi ya Juu ya Wanawake ya China ya Wuhan Jianghan University.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atahamia London mnamo Oktoba kufuatia kumalizika kwa Michezo ya Asia na Uchina.Kuhama kwake kunategemea kibali cha kimataifa na kupata kibali cha kufanya kazi.

Afisa mkuu mtendaji wa Arsenal Vinai Venkatesham ataachia majukumu yake msimu ujao wa joto baada ya miaka 14 na klabu hiyo.

Alisema: “Huu ulikuwa uamuzi mgumu, lakini ni wakati wa kutafuta changamoto nyingine. Sasa sio wakati wa kuagana kwani ninabaki nikizingatia hadi siku yangu ya mwisho na kuunga mkono mabadiliko ya bila mshono.

Mwenyekiti Mwenza Josh Kroenke alitoa maoni: “Bodi inaunga mkono kikamilifu nia ya Vinai ya kutekeleza changamoto yake inayofuata.

Julian Draxler anatarajiwa kujiunga na klabu ya Qatar Al-Ahli SC kutoka Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa Sky .

Vilabu hivyo vinakaribia kukamilisha dili la thamani ya zaidi ya £17.2m (€20m).

Draxler anatarajiwa kusaini mkataba hadi 2025.

TH

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mkufunzi wa Jamhuri ya Ireland Stephen Kenny atasalia kuwa kocha kwa muda uliosalia wa kampeni za Euro 2024, Chama cha Soka cha Ireland kimesema.

Shinikizo iliongezeka kwa Kenny baada ya kushindwa Jumapili na Uholanzi ilimaliza kabisa matumaini ya Jamhuri ya Ireland ya kufuzu kwa fainali za mwaka ujao.


Chanzo: BBC

Post a Comment

0 Comments