Ngozi inaweza kueleza afya yako ya ndani

 

fdc

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGE

  • Author,Zaria Gorvett
  • Nafasi,BBC Future

Mikono yangu na kiwiliwili vimefunikwa kabisa na fulana ya mikono mirefu - kinga dhidi ya jua, huku kichwa changu kikiwa kimefunikwa na kofia kapelo - ili kulinda uso wangu. Ni juhudi za kuepuka kuzeeka zaidi kunakosababishwa na jua.

Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa ngozi yetu inaeleza mambo mengi kuhusu mitindo yetu ya maisha; inaonyesha athari ya kuvuta sigara, kunywa pombe, kuchomwa na jua na kuishi maisha ya dhiki.

Utafiti wa Baltimore Longitudinal ulifuata maelfu ya wanaume - watu wazima (na baadaye wanawake) kwa miongo kadhaa, ili kuona jinsi afya zao zilivyobadilika, na jinsi zilivyoathiriwa na jeni na mazingira yao.

Miongo miwili tu baadaye, wanasayansi walikuwa tayari wamefanya uvumbuzi wa kuvutia - wanaume wasio na utulivu wa kihisia wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa moyo.

Matokeo ya kushangaza zaidi yalithibitisha kile ambacho kimeshukiwa kwa muda mrefu; jinsi unavyoonekana ni kipimo sahihi cha afya yako ya ndani.

Kufikia 1982, wanaume ambao mwanzoni mwa utafiti walionekana kuwa wakubwa kwa umri wao walikuwa na uwezekano mkubwa wa kufa miaka 20 baadaye. Hii inaungwa mkono na utafiti wa hivi karibuni zaidi, ambao uligundua kuwa wagonjwa ambao wanaonekana wamezeeka miaka 10 kuliko wanavyopaswa, 99% wana na matatizo ya afya.

Afya ya ngozi inaweza kutumika kutabiri idadi ya kadhaa ya matatizo ya kiafya.

Umri wako na ngozi yako

sdwq

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGE

Kuna njia kuu mbili za kupima umri wa mtu. Ya kwanza ni ile ya kawaida. Lakini pia kuna umri wa kibiolojia, ambayo inaonyesha kiwango chako cha unazeeka kimwili (ukomavu wa viungo vyako na seli).

Lakini ni mazingira kusababisha uharibifu ngozi. Mionzi ya ultraviolet B (UVB) inaweza kuharibu DNA - kusababisha saratani ya ngozi. 95% ya mionzi ya ultraviolet inayofika kwenye uso wa dunia ni ultraviolet A (UVA). Miale ya jua inaweza kupenya ndani kabisa ya ngozi. Ultraviolet unahusishwa na zaidi ya 80% ya mabadiliko yanayoonekana kwenye ngozi.

Mwaka 2000, dhana mpya iliibuka, kikundi cha wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Bologna, Italia, kilipendekeza njia mpya ya kufikiria kuhusu kuzeeka.

Tukiwa vijana kinga za mwili huzalishwa ili kudumisha utaratibu. Lakini kadiri tunavyozeeka uzalishwaji huu huja na kemikali zenye nguvu katika mwili na, kuharibu seli zenye afya. Vilevile kemikali tunazotumia hupunguza unene wa ngozi, kuzalisha makunyanzi, na kupunguza unyumbufu wa ngozi.

Kwa upande mwingine kemikali inayotolewa na ngozi ikiwa haina kazi huingia kwenye damu, ambapo huenea na kuharibu tishu nyingine. Kemikali kutoka kwenye ngozi zinaweza kufikia na kuharibu viungo vinavyoonekana kuwa havihusiani, kutia ndani moyo na ubongo.

Matokeo yake ni kuzeeka kwa kasi na hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa. Ngozi iliyozeeka au yenye ugonjwa imehusishwa na magonjwa ya moyo na mishipa, kisukari cha aina ya 2 na kupungua uono, pamoja na ugonjwa wa magonjwa mengine.

Ingawa sote tunafahamu hatari za kuvuta sigara, kunywa pombe, kula kupita kiasi na kutofanya mazoezi, inaweza kusemwa kuwa afya mbaya ya ngozi inaweza kuchangiwa navyo.

Kulinda ngozi

sdw

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGE

Hatua ya kwanza ya kulinda ngozi ni kujikinga na jua. Kuvaa shati, kupaka mafuta, kuvaa kofia kapelo, miwani ya jua, na kupata mahali kwenye kivuli.

Kulinda ngozi yako kutokana na jua ni bora sana katika kuzuia dalili zinazoonekana za kuzeeka. Pia, kujilinda kunazuia maambukizi mengi ya mionzi wakati unazeeka na magonjwa ya uzeeni.

Lakini hii sizo njia pekee za kuweka ngozi yako katika hali nzuri. Njia rahisi zaidi ya kuboresha afya ya ngozi ni kupaka mafuta. Na kuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba hii inapunguza magonjwa ya ngozi.

Mbali na kuwa na mikunjo isiyosawazika, ngozi iliyozeeka na jua huwa kavu zaidi. Viwango vya unyevu kwenye ngozi hufika kilele ukiwa na umri wa miaka 40. Wakati ngozi yetu imekauka kazi zake za kuzuia maambukizi na sumu za mazingira inakuwa ngumu zaidi.

Viungo vingi vya asili vinaweza kusaidia. Kunywa maji zaidi kunaweza kusaidia kuweka ngozi yako na unyevu zaidi. Kwa hivyo kuilinda ngozi kuna faida yake, lakini usisahau kuipa unyevu pia.

Chanzo: BBC Swahili





Post a Comment

0 Comments