Tetesi tano kubwa za soka

 

Jadon Sancho na Erik ten Hag


Winga wa Manchester United Jadon Sancho leo ameripotiwa kufika kwa mazoezi kwenye kambi ya Manchester United ya Carrington lakini, kama Simon Stone anavyosema, huenda pengine mambo yamebadilika la sivyo basi atakuwa akifanya mazoezi nje ya kikosi cha kwanza.

Je, Erik ten Hag amekuwa mkali sana kwa winga huyo? Je, Sancho alikuwa sawa kuelezea kutofuridhishwa kwake na hatua ya kuachwa nje ya kikosi cha kwanza wakati wa mchezi ya United dhidi ya Arsenal?

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik ten Hag amethibitisha kuwa wachezaji wawili wa safu ya ulinzi Lisandro Martinez na Victor Lindelof wako katika hali nzuri kucheza mechi ya kesho ya Ligi ya Premia dhidi Brighton.

Beki Raphael Varane na kiungo Mason Mount hawapatikani lakini "wapo mahali pazuri".

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp anasema Thiago Alcantara anagombea tena, wakati Ibrahima Konate amekuwa akifanya mazoezi siku mbili zilizopita.

Kuhusiana na kikosi chake baada ya dirisha la usajiliali anasema: "Tuko sawa. Nimekuwa na wachezaji wa safu ya kati kwa miaka mingi. Walikuwa wachezaji wa hali ya juu, Ilikuwa changamoto kubwa kuwabadilisha lakini naridhika na wale nilio nao sasa."

Thiago

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Thiago

Everton wako katika hali mbaya ndani na nje ya uwanja, wakiponea chupuchupu kushuka daraja katika misimu miwili iliyopita, ikiwa ni pamoja na kusalia na ushindi katika siku ya mwisho muhula uliopita.

Mwezi ujao klabu hiyo itafika mbele ya tume huru kwa madai ya kukiuka sheria za Ligi ya Premia ya Uchezaji wa Haki ya Fedha, lakini Everton wamekanusha makosa hayo na kusema "wako tayari kutetea kwa dhati" msimamo wao.

tt

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,

Romeo Lavia

"Romeo Lavia alikuwa akifanya mazoezi vizuri wiki iliyopita lakini aliumia kifundo cha mguu wakati wa mapumziko ya kimataifa kwa hiyo tunasubiri Jumatatu ili kujua litakalofuata, amesema mkufunzi wa Chelsea Mauricio Pochettino.

"Ni hali ya kusikitisha kwa sababu alikuwa anakaribia kuwa tayari kucheza.

Chanzo: BBC Swahili 

Post a Comment

0 Comments