Ole Gunnar Solskjaer: Meneja wa Manchester United asema hatua zichukuliwe kudhibiti chuki mitandaoni

Paul Pogba (left) and Manchester United manager Ole Gunnar SolskjaerHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPaul Pogba alikosa kufunga mkwaju wa penalti katika mechi iliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Wolves
Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema makampuni ya mitandao ya kijamii ni lazima yasitishe kusambaa kwa chuki baada ya mchezaji wake wa kiungo cha kati Paul Pogba kukabiliwa na ubaguzi katika mitandao wiki iliyopita.
Raia huyo wa Ufaransa amekuwa mchezaji wa tatu katika wiki moja kukabiliwa na ubaguzi wa rangi katika majukwaa hayo ya kijamii baada ya kukosa kufunga bao la penalti katika mechi dhidi ya Wolves.
"Paul ni kijana mahiri - inamfanya kuwa mkakamavu zaidi," amesema raia huyo wa Norway.
"Ni lazima tufanye jambo kuhusu hili na maafisa husika ni lazima walishughulikie."
Manchester United midfielder Paul PogbaHaki miliki ya pichaPA MEDIA
Solskjaer ndio mtu wa hivi karibuni kutoka klabu hiyo kuitisha hatua kali zichukuliwe baada ya mlinzi Harry Maguire na mshambuliaji Marcus Rashford. Aliyekuwa mlinzi wa klabu hiyo Phil Neville pia amependekeza kuwa wachezaji wajitoe katika mitandao ya kijami kama njia ya kulalamika yaliotokea.
"Mitandao ya kijamii ni sehemu ambayo Harry [Maguire] amesema watu hujificha kwa utambulisho bandia - sio uamuzi wangu ku kuyabadili," ameongeza Solskjaer, ambaye pia amesema wachezaji hawatopigwa marufuku kutumia mitandao ya kijamii.
Wiki iliyopita, Chelsea ilishutumu "ujumbe wa matusi" uliomlenga Tammy Abraham baada ya kushindwa kufunga mkwaju wa penalti katika fainali ya Super Cup dhidi ya Liverpool. Alafu Jumapili, mshambuliaji wa Reading Yakou Meite alishutumu matusi ya kibaguzi dhid iyake kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuokolewa mkwaju.
Mapema wiki hii, Twitter ilibaini kuwa itakutana na wawakilishi wa United na wanaharakati wa kupambana na mashambulio ya matusi Kick It Out.
Manchester United manager Ole Gunnar SolskjaerHaki miliki ya pichaREX FEATURES
'Hakuna vita kati ya Pogba and Rashford'
Wakati huo huo, Solskjaer amesema hatobadili sera yake ya penalti mara mbili baada ya kuhustumiwa mbinu zake alizotumia katika mechi iliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Wolves.
Huku ikiwa na nafasi ya kuishia kwa ushindi wa 2-1 katika mechi hiyo, Pogba alishinda penalti na baada ya majadiliano na Rashford, aliamua kwamba atasukuma tobwe, jitihada ambazo ziliokolewa na Rui Patricio. Wiki moja kabla ya hapo, Rashford alifanikiwa kusukuma tobwe la aina hiyo katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Chelsea.
Solskjaer amesema: "Nina hakika mutamuona Pogba akiifungia United bao jingine tena.
"Musishangazwe iwapo Marcus au Paul wakifunga bao linalofuata. Hakuna vita baina yao."

Post a Comment

0 Comments