Benjamin Netanyahu: Israel itazichukua ardhi za makaazi ya Wayahudi ukingo wa magharibi


Bwana Netanyahu alitangaza kuhusu mipango yake kabla ya kufanyika kwa uchaguzi katika runinga siku ya JumanneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mataifa ya Arabuni yameshutumu mpango wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wa kunyakua eneo moja katika eneo la ukingo wa magharibi.
Siku ya Jumanne bwana Netanyahu aliomba kutumia uhuru wa Israel kuliteka bonde la Jordan na kaskazini mwa Dead Sea iwapo atachaguliwa tena kufuatia uchaguzi mkuu wiki ijayo.
Maafisa mjini Jordan , Uturuki na Saudia walikosoa tangazo hiilo.
Utekaji huo uliopendekezwa na Bwana Netanyahu utakuwa uhalifu wa kivita na kwamba utaangamiza fursa zozote za amani , alisema Saeb Erekat.
Muungano huo wa mataifa ya Arabuni umeshutumu hatua za uchokozi zinazofanywa na Israel ukisema ni kitendo cha hatari.
Israel imekuwa ikikalia eneo la ukingo wa magharibi 1967 lakini haijataka kujiongezea ardhi. Palestina inalidai eneo hilo lote ili kuanzisha taifa huru siku zijazo.
Bwana Netanyahu alisisitiza kuwa Israel itaendelea kukalia eneo hilo la bonde la Jordan kwa maswala ya kiusalama.

Je Benjamin Netanyahu alisema nini?

Bwana Netanyahu ambaye alikuwa akifanya kampeni za uchaguzi alizindua mpango huo katika runinga.
Alisema kwamba atayachukua makaazi yote yanayokaliwa na Wayahudi katika eneo la ukingo wa magharibi, lakini hilo litalazimika kusubiri hadi kutakapofanyika uchapishaji wa mipango ya rais Donald Trump kuhusu mpango wa amani katika Israel na Palestina.
Kuna eneo moja ambalo tunaweza kuonyesha uhuru wetu mara moja baada ya uchaguzi , bwana Netanyahu alisema kuhusu bonde hilo la Jordan na kaskazini mwa Dead Sea. iwapo nitapokea kutoka kwenu amri ya kufanya hivyo.
Ramani ya West Bank
Waziri mkuu anaongoza chama cha mrengo wa kulia cha Likud , ambacho kwa sasa kinakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka chama cha upinzani chenye msimamo wa katikati wa muungano wa Blue and White.
Uchaguzi utafanyika Jumanne ijayo , baada ya Netanyahu mapema mwaka huu kushindwa kuunda muungano kufuatia kura nyengine iliofanyika.
Mwandishi wa BBC katika eneo la mashariki ya kati Tom Bateman , anasema kwamba tangazo hilo la waziri mkuu huenda likamsaidia kupata uungwaji mkono kutoka kwa raia wa mrengo wa kulia.
Kiongozi mwenza wa muungano wa Blue and White , Yair Lapid, alimshutumu bwana Netanyahu, akisisitiza kuwa hataki kunyakua ardhi bali anataka kuchukua kura.
''Huu ni ujanja wa uchaguzi na sio hata ujanja ambao utafanikiwa kwa kuwa uongo wake upo wazi'' , alisema.
Baadaye siku ya Jumanne ,bwana Netenyahu alitoroshwa na walinzi wake katika ukumbi mmoja wakati wa kampeni katika eneo la Ashdod , mji wa kusini huku ving'ora vya mashambulizi ya angani vikilia.
Israel inasema kua ilishambulia roketi mbili ambazo zilikuwa zimerushwa na Wapalestina kutoka eneo la mkanda wa Gaza , ikiwemo kifaa cha silaha.

Je wengine wanasemaje?

Muungano wa mtaifa ya Arabuni unasema kwamba mipango ya bwana Netanyahu itakiuka sheria za kimataifa na kuvuruga msingi wa amani.
Afisa mwandamizi wa Palestina Hanan Ashrawi alisema kuwa mipango hiyo haiuliziki na ni tishio la amani ya kimataifa na usalama.
''Tangazo hilo ni la vita dhidi ya haki za raia wa Palestina pamoja msingi wa sheria ya uongozi'' , alisema.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Jordan , Ayman Safadi, aliutaja mpango huo kama uchochezi mbaya na kuonya kwamba huenda likalishinikiza eneo lote kuingia katika ghasia.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Uturuki Mevlut Cavusoglu, aliitaja ahadi hiyo kuwa ya kibaguzi na kumkosoa bwana Netanyahu kwa kutoa kila ujumbe wa uchochezi kabla ya uchaguzi huo.
Waziri mkuu wa Palestina Mohammed ShtayyehHaki miliki ya pichaREUTERS
Saudi Arabia pia ilishutumu tangazo hilo katika vyombo vya habari kama uchochezi hatari na kutoa wito kwa kufanyika kwa mkutano wa dharura wa mawaziri wa maswala ya kigeni ya mataifa 57 wanachama wa shirika la ushirikiano wa Kiislamu.
Je ni nini chanzo cha swala hilo la eneo la ukingo wa magharibi?
Ukubwa wa Bonde la Jordan na kaskazini mwa bahari ya Dead Sea unajumlisha thuluthi moja ya eneo la West bank.
Israel ilikalia eneo la ukingo wa magharibi , pamoja na mashariki mwa Jerusalem , Gaza na milima ya Golan iliopo Syria miaka ya 1967 wakati wa vita vya mashariki ya kati.
Ilinyakuwa eneo la mashariki mwa Jerusalem , 1980 na milima ya Golan 1981 ijapokuwa hakuna hatua iliokubalika kimataifa kwa miongo kadhaa.
Makaazi ya West Bank
Utawala wa rais Trump umeidhinisha hatua zote mbili ikibadilisha sera ya awali ya Marekani .
Bado haijulikani iwapo itapigania suluhu ya mataifa mawili yalio huru- mpango ambao umetawala juhudi za kidiplomasia za kuafikia amani katika eneo hilo.
Hatma ya eneo la ukingo wa magharibi linatokana na mzozo wa Israel na Palestina.
Israel imejenga makaazi 140 katika eneo hilo na mashariki mwa Yerusalemu ambayo hudaiwa kuwa haramu chini ya sheria ya kimataifa ijapokuwa Israel inapinga wazo hilo.

Post a Comment

0 Comments