Programu ya ngono inatumika kwenye Facebook

Woman with calendar

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionProgramu ya mzunguko wa hedhi
Taarifa binafsi na siri zikiwa pamoja na wakati ambao watu wanafanya mapenzi zinaonyeshwa katika mtandao wa Facebook, utafiti uliofanywa 'Privacy International' umeeleza.
Utafiti huo umeonyesha namna ambavyo programu iliweza kuona taarifa zote ambazo ziliandikwa katika mitandao.Hii ikijumlisha taarifa kama ya siku ambazo mtu alitumia dawa za mpango wa uzazi, siku zake za hedhi na dalili alizokuwa anazipata.
Tangu utafiti huo ufanyike, programu moja imesema kuwa imebadili sera zake za siri.
Sample of what Facebook is sent from a period tracking appHaki miliki ya pichaPI
Image captionvitu ambavyo Facebook inaviona - "Lengo : Kupata ujauzito"
Programu ya mzunguko wa hedhi inahifadhi taarifa ambazo ni binafsi sana kwa mtu kama vile hali ya afya yake, ngono, hisia zake, chakula anachokula na pedi anazotumia.
Na pogramu hiyo huwa inamuelekeza siku za miezi ambazo anatarajia kupata hedhi yake.
Kushirikisha Facebook kwa kutumia programu kunaweza kufanya wapate fedha kutokana na matangazo ambayo yanawekwa.
Screen grab of data chart from PIHaki miliki ya pichaPI
Image captionProgramu ya Maya inawahamasisha watumiaji wa programu yao kuingiza taarifa za jinsi wanavyojisikia na kuweka kwenye Facebook
BBC imejaribu kuwasiliana na kampuni hizo na hakuna aliyetoa jibu lolote.
Utafiti huo unaamini kuwa hilo suala linaleta hofu kwa watumiaji wa programu hizo kwa kuwa umeshindwa kutunza siri za taarifa zao.
Na wa husika wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwaaminisha watumiaji jambo ambalo si la kweli.
Facebook imetangaza kuanzisha programu yake na kuachana na biashara za kushirikiana na wengine katika mtandao huo.

Post a Comment

0 Comments