Serikali yaanza kuvifufua viwanda vya kuchakatwa Mifugo


Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma

Serikali imesema imeanza michakato wa kuvirudisha serikalini viwanda kuchakatwa Mifugo vilivyokuwa vikimilikiwa na watu binafsi na kushindwa kuviendeleza ili kuhakikisha watanzania wananufaika na ufugaji wanaofanya kuchakatwa hapahapa.

Hayo yamebainishwa leo bungeni na Naibu waziri ya Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu Felista Bula aliyehoji ni lini serikali itaanzisha viwanda vya kuchakatwa Mifugo ili wafugaji wanufaike na kazi zao.

Amesema tayari serikali imeanza kurudisha viwanda vilivyokuwa viki nilikuwa na watu binafsi na kushindwa kuendelezwa, ametolea mfano kiwanda Cha TMC kilichopo Dodoma kimeridhishwa na Sasa kinaendelea kufanya kazi vizuri.

Amebainisha kuwa pia kiwanda Cha Tanganyika Pekers cha Shinyanga nacho kimeanza kufanya kazi na kuhudumia wakazi na wafugaji wa Kanda ya ziwa, sambamba na hilo wameanza kukifufua kiwanda cha Ruvu nacho kianze kufanya kazi.

Amesema pia vipo vya wazalando ambao ambao vinafanya kazi akatolea mfano kiwanda Cha Chobo Investment kilichopo Mwanza nacho kinafanya kazi na kinauwezo wa kuchakatwa ng'ombe mia tano (500) na mbuzi elfu moja(1000).

Post a Comment

0 Comments