tangazo

Beki wa Tunisia ahukumiwa kwenda jela

Beki wa zamani wa club ya Zamalek ya Misri Hamdi Nagguez ,27, amehukumiwa kifungo cha miezi minne jea kwa kosa la kumtolea hadharani lugha ya matusi.

Hamdi amepewa adhabu hiyo sambamba na faini ya dola 35,000 (Tsh milioni 80) sababu ya kumtukana afisa wa umma wa wizara ya mambo ya ndani ya Tunisia baada ya kuombwa leseni ya gari na kukutwa hana wakati kukiuka na zuio la serikali.

Kosa hilo Hamdi alitenda April 22  akiwa Tunisia katika mji wa Sousse, kama utakuwa unakumbuka vizuri Hamdi alicheza kwa miaka miwili Zamalek kabla ya December 2019 kuamua kuvunja mkataba na kurejea kwao sababu kutokulipwa malimbikizo ya mishahara yake.

Post a Comment

0 Comments