Madagascar yaendelea kusambaza shehena ya dawa ya Corona

Madagascar ambayo imetangaza kugundua dawa ya asili ambayo inatibu ugonjwa wa corona, imeendelea kushafirisha shehena na dawa hiyo nje ya nchi licha ya jumuiya ya kimataifa pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) kutoa tamko la kutoitambua dawa hiyo.

Ndege za nchi hiyo zinashiriki katika zoezi hilo la kusafirisha dawa hiyo kulingana na mahitaji ya wateja.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo, baadhi ya nchi zilioonesha utayari wa kuchukua dawa hizo ni pamoja na Senegal, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Tanzania.

Wakati nchi hizo zikionesha nia, tayari Guinea Bissau imepokea mzigo wa dawa, kwa ajili ya kutumiwa na wananchi wake.

Akizungumza akiwa Chato mkoani Geita, Rais John Magufuli amesema kuwa tayari Madagascar imeandika barua kuhusu uwepo wa dawa hiyo, na kwamba Tanzania itatuma ndege kwenda kuchukua.

Post a Comment

0 Comments