tangazo

Mapenzi hayajawahi kunipa stress- Mimi Mars


Chugga Queen kutoka lebo ya Mdee Music, msanii Mimi Mars ameibuka na kusema kuwa mapenzi ni kitu ambacho hakijawahi kumpa msongo wa mawazo (stress).

Mimi Mars ambaye jina lake halisi ni Marianne Namshali Mdee, amefunguka hayo kupitia Insta Live baada ya kuulizwa iwapo amewahi kushauriwa na dada yake, Vanessa Mdee pale anapokuwa ameumizwa kwenye mahusiano.

ADVERTISEMENT


“Kwanza sijawahi kuwa stress kwa sababu ya mapenzi, tuanzie hapo, wala huwa silii,” amejibu Mimi Mars ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la Una.

Mimi Mars ambaye mbali na kuwa msanii wa muziki, mrembo huyo ni Muigizaji wa filamu na tamathilia pia ni Mtangazaji wa TV.

 Itakumbukwa, aliwahi kuweka wazi kupitia kipindi cha Chill Na Sky hawezi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mtu aliyepo kwenye tasnia ya muziki wala filamu nchini.

Post a Comment

0 Comments