tangazo

Rais wa Madagascar abadili msimamo kuhusu dawa ya mitishamba ya kutibu corona

Sina mpango wa kuanzisha sindano za dawa ya mitishamba', asema Rajoelina
Mwezi uliopita bwana Rajoelina alizindua rasmi dawa ya mitishamba ambayo alisema kwamba ina uwezo kuzuia na kuponya wagonjwa walio na virusi vya corona.
lakini hilo lilipingwa na shirika la afya duniani kwasababu hakuna thibitisho la kisayansi kuhusu dawa hiyo.
Taasisi ya kitaifa ya matibabu nchini Madagascar pia ilitilia shaka uwezo wa dawa hiyo iliotengenezwa kutoka kwa mmea wa pakanga, ikisema huenda ikaathiri afya ya wanadamu.
Lakini licha ya taarifa ya taasisi hiyo , siku ya Jumanne bwana Rajoelina alisema kwamba Madagascar itaanzisha sindano za dawa hiyo huku akiongezea kwamba majaribio yake tayari yameanza kufanywa nchini Marekani.
Hatahivyo Michelle Sahondrarimalala, ambaye ni daktari na mkurugenzi wa tafiti za idara ya mahakama, amefafanua zaidi alichomaanisha rais huyo, akisema kwamba waandishi hawakumuelewa kile ambacho kiongozi huyo wa taifa alitaka kutangaza.
Alisema kwamba hakukuwa na fikra zozote za kuiweka dawa hiyo kutumika kupitia sindano na kwamba kamati ya kisayansi haijafikia uamuzi kama huo.

Je umoja wa Afrika ulisema nini?

Umoja wa Afrika (AU) ulisema unafanya mazungumzo na Jamuhuri ya Madagascar, ili kupata data za kiufundi kuhusu usalama na ufanisi wa dawa hiyo.
Baada ya kupata maelezo Umoja huo kupitia kituo chake cha udhibiti wa magonjwa - (Africa CDC), utatathimini data zilizokusanywa kuhusu usalama na ufanisi wa tiba hiyo.
WHO: Msiziamini dawa za mitishamba
Hatahivyo Shirika la Afya Duniani limesihi watu kutoweka imani zao kwa dawa za mitishamba zinazotengenezwa na wenyeji kwa misingi ya kudai kukabiliana na virusi vya corona.
Hatua hiyo inawadia wakati ambapo marais karibu wanne wa Afrika walidaiwa kuagiza kiasi kikubwa cha dawa hiyo.
Shirika la Afya Duniani lilitoa onyo hilo wakati ambapo kila mmoja duniani ana hamu ya kupata dawa ya kutibu virusi vya corona.
WHO lilisema ni muhimu dawa zinazosemekana kuwa na uwezo wa kutibu corona kufanyiwa majaribio ya kisayansi kabla ya kutumika .

Mataifa ya Afrika yaagiza dawa ya Madagascar

Lakini taarifa hiyo ilipuuzwa na baadhi ya viongozi wa Afrika.
Marais wa Tanzania, Jamuhuri ya Congo, Guinea Bissau na Equatorial Guinea wote waliamua kutuma ndege nchini Madagascar kuchukua dawa hiyo ya mitishamba.
Dawa hiyo inayohusishwa na mmea wa Kichina unaoitwa Artemisia(pakanga)-ambao ni mojawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria.
Tanzania kuichunguza dawa ya mitishamba kutoka Madagascar
Baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi kwenda Madagascar kuichukua dawa hiyo ya mititishamba, Tanzania sasa imesema dawa hiyo itachunguzwa zaidi.
Mkuu wa Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) chini humo Profesa Yunus Mgaya alisema kuwa dawa hiyo itafanyiwa uchunguzi wa kikemia na wa kibaiolojia kubaini utendaji wake.
Virusi vya corona: Je, Madagascar wamepata dawa ya mitishamba kutibu virusi vya corona?
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Paramagamba Kabudi ambaye alikwenda Madagascar kuchukua dawa hiyo alisema:''Hatujachukua dawa kutoka kwa sangoma'' na kuongeza kuwa:''Nilikwenda Madagascar kwa ndege ya rais kupokea zawadi kutoka nchini Madagascar ''
Rais Magufuli aliniruhusu niende na wataalam, na tulipofika kule walikua na mkutano wa saa nne wa kuzungumza na wenzao kuhusiana na dawa hii '', amesema Profesa Kabudi.
lakini rais huyo wa Madagascar Andry Rajoelina hakusita hapo katika kuikuza dawa hiyo kwani pia aliwakosoa wakosoaji wa dawa hiyo ya mitishamba akisema ni tabia ya ubwenyenye wa mataifa ya magharbi dhidi ya Afrika.
''Iwapo ingekuwa ni taifa la Ulaya ambalo liligundua dawa hiyo , je kungekuwa na wasiwasi? sidhani'', bwana Rajoelina alisema katika mahojiano na shirika la habari la ufaransa 24.

Post a Comment

0 Comments