"Silinde hajaandika barua ya kujiuzulu" - Bulaya

Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya, amesema kuwa Mbunge wa Momba David Silinde, hajaandika barua ya kujiuzulu isipokuwa kaamua kuachia ngazi baada ya Wabunge wenzake kutokuwa na imani naye, kwani alikiuka maagizo ya Mwenyekiti wa chama hicho.

Bulaya ameyabainisha hayo leo Mei 6, 2020, wakati wa mazungumzo maalum na kipindi cha Supa Breakfast ya East Afrika Radio na kusema kuwa kama angekuwa ameandika barua basi yeye kama mnadhimu angeipata.

"Kwanza nikanushe Shilinde hakuandika barua na kama angeandika mimi kama mnadhimu ningeipata, yeye ni Katibu wa Wabunge na ameupata baada ya kupigiwa kura, sasa Wabunge waliowachagua hawana tena imani nao ni Wabunge ndiyo wamemfurusha kazi kwa usaliti wake, baada ya kuona wabunge wamechachamaa ndiyo kaamua kutumia kivuli cha ku-resign" amesema Ester Bulaya.

Mbunge Silinde alidai kuwa tayari amekwishamuandikia barua ya kujiuzulu, Mwenyekiti wa chama chake Freeman Mbowe, huku Ester Bulaya naye akikanusha kuwa Shilinde hajaandika barua yoyote ile.

Post a Comment

0 Comments