tangazo

Sumalee kuwakutanisha Alikiba na Diamond kwenye Qaswida

Hitmaker wa Hakunaga, Sumalee,  aahidi kuwaleta wasanii Alikiba na DiamondPlatnumz kwenye Qaswida moja.

Akizungumza leo Kupitia kipindi cha The Switch cha WasafiFm, Suma Lee amesema miongoni mwa mambo anayohitaji kuyatimiza ni kuwaimbisha Qaswida wakali wawili wa Bongo Fleva Alikiba na Diamond Platnumz

"Nitaimba Qaswida na Diamond pamoja na AliKiba, iwe Qaswida moja ama kila mtu na ya kwake... wataimba iwe kilazima, kihiari, nitaimba nao. Wataimba Qaswida". Alisema Maalim Sumalee.

Itakumbukwa, kabla ya kuachana na BongoFleva, SumaLee aliwahi kutamba na kibao chake cha Hakunaga lakini kwa sasa ana zawadi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan aliyoiachiwa mapema wiki hii inaitwa YaRasulallah.

Post a Comment

0 Comments