tangazo

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 04.05.2020: Rakitic, Pogba, Ndombele, Pedro, Mkhitaryan, Bakayoko

Ivan Rakitic amekuwa akichezea Barcelona tangu 2014
Tottenham inaongoza katika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajilikiungo wa kati wa Barcelona na Croatia, 32, Ivan Rakitic. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Inter Milan inataka kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 27. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Paul PogbaHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionPaul Pogba alikuwa kama mchezaji wa akiba katika mechi dhidi ya Watford na Newcastle aliporejea baada ya kuuguza jeraha kwa miezi mitatu
Mshambuliaji wa Chelsea na Uhispania Pedro, 32, anawindwa na Roma na Real Betis. (Goal)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 23, yuko tayari kusalia na kupigania nafasi yake katika timu licha ya kwamba Barcelona imeonesha nia ya kutaka kumsajili
Tanguy Ndombele,Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionNdombele akiichezea Tottenham katika Ligi ya Primia
Mchezaji wa Real Madrid na winga wa Uhispania Lucas Vazquez, 28, anasema wazo la kucheza na klabu cha Uingereza ni jambo linalomfurahisha. (Guardian)
Henrikh MkhitaryanHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHenrikh Mkhitaryan mchezaji wa Arsenal anayechezea Roma kwa mkopo
Arsenal iko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Armenian Henrikh Mkhitaryan msimu huu ili kupata pesa. Mchezaji huyo, 31 kwasasa yuko Roma kwa mkopo. (Mirror)
Arsenal na Chelsea zote zinataka kumsajili kiungo wa kati wa klabu ya Feyenoord raia wa Uturuki Orkun Kokcu, 19. (Express)
Tiemoue BakayokoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTiemoue Bakayoko amewahi kuchukua taji la Ufaransa akiwa Monaco
Sevilla inammezea mate kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko. Mchezaji huyo wa miaka 25 yuko kwa mkopo Monaco kutoka Chelsea. (France Football - in French)
Ibrahima Konate,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionIbrahima Konate anawindwa na Manchester United
Manchester United imewasiliana na mwakilishi wa RB Leipzig wa Ibrahima Konate, 20. (Le10 Sport - in French)
Aliyekuwa mchezaji wa Machester United na Uholanzi Jaap Stam, 47, anasema amefanya mazungumzo na FC Cincinnati ya kuwa kocha mpya wa timu hiyo. (Goal)

Post a Comment

0 Comments