tangazo

TRA Rukwa yakamata Sukari na Pombe kali zenye thamani ya milioni 6

Mamlaka ya mapato nchini TRA mkoa wa Rukwa imeendesha msako wa siku nne na kukamata bidhaa zilizoingizwa nchini kinyume cha sheria ambazo ni sukari tani mbili na pombe kali za aina tofauti zenye thamani ya shilingi milioni 6.

Akitoa taarifa ya msako huo meneja wa TRA mkoa wa Rukwa, Fredrick Kanyilili amesema msako huo uliendeshwa katika miji midogo yote na vijiji vya mpakani na kuwatia nguvuni watuhumiwa watano waliokutwa na sukari na pombe kali kutoka nje ya nchi iliyoingizwa nchini bila kufuata utaratibu.

Aidha Kanyilili ametoa onyo kwa wafanya biashara wanaotaka kujipatia faida kubwa kwa kuuza bidhaa kutoka nje ya nchi bila kuzilipia ushuri wa forosha.

Post a Comment

0 Comments