tangazo

Wagonjwa wa Corona wapungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini


Serikali imetoa hali mwenendo wa wagonjwa wa Corona ambao walikuwa wametolewa taarifa hapo awali kuwa na maambukizi ya virus hivyo hapa nchini na kusema idadi hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa sana tofauti na hali ilivyokuwa hapo mwanzo.

Takwimu hizo zimetolewa Jijini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa ibada ya swala ya iddi iliyofanyika katika msikiti wa Gadafi jijini humo.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema maambukizi hayo yamepungua kwa kasi kikubwa sana na baadhi ya hospitali hizo kubaki na wagonjwa wachache Sana na nyingine kutokuwa na wagonjwa kabisa, katika hospitali zote hasa jiji la Dar es saalam lililokuwa na wagonjwa wengi.

Akitoa idadi hiyo amesema " mfano hospitali ya Amana ina mgonjwa 1, Hospitali ya mloganzira ni kubwa lakini tulitenga sehemu ndogo pembeni napo amebaki mgojwa mmoja, temeke hamna mgojwa na kwenye hospitali za binafsi ambazo zilituunga mkono nyingi hazina wagonjwa, wagonjwa wamebaki Aghakani na inawagonjwa 11 tu" amesema Mhe Majaliwa.

Amesema katika maeneo yote yaliyokuwa na wagojwa idadi imepungua kwa kasi na nyingine hazina wagonjwa kabisa, akitolea mfano kituo Cha afya Mkonze kilichokuwa na wagonjwa 12 na sasa Kuna wagonjwa 3 tu.

Amewapongeza viongozi wa dini zote kwa kuungana na wito wa Mheshimiwa Rais Dkt John Magufuli wa kuliombea taifa ili kuweza kuepukana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Amewataka watanzania kutobweteka na kupungua kwa maambukizi hayo bali waendelee kuchukua tahadhari zaidi ili ugonjwa huo uweze kutokomezwa kabisa hapa nchini, sambamba na kuendelea kuliombea taifa na kuchukua tahadhari zinazotolewa na wataalamu.

Pia amewahimiza wanafunzi wanaonza masomo juni mosi mwaka huu kuchukua tahadhari zote zinazotakiwa kwani wao ndio itakuwa mwanga kwaajili ya kuruhusu na wengine wa ngazi za chini kuendelea na masomo.

Pia amevipongoze vyombo vya habari kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuelimisha umma namna bora ya kujikinga na virusi vya Corona kwani Sasa mpaka vijijini elimu imewafikia na wanatambua athari za ugonjwa huu.

Kwa upande wake shekhe Mkuu wa Mkao wa Dodoma, Mustaafa Rajabu, amepongeza Rais Dkt John Magufuli kwa ujasili alionao pamoja na namna alivyolishugurikia gonjwa hilo hasa kwa kumtamguliza Mungu mbele katika mapambano hayo.

Pia amehimiza waislamu wote kwenda kuyaishi yake yote mazuri waliojifunza katika kipindi hiki Cha mfungo na kuacha mambo ya anasa ambayo yatakwenda kuharibu ibada zao.

Post a Comment

0 Comments