tangazo

Waziri Aweso: Watumiaji wa maji washirikishwe usomaji wa Mita

Serikali imewaagiza wakurugenzi wa mamlaka zote za maji nchini wahakikishe watumiaji wa maji wanashirikishwa kikamilifu katika usomaji wa mita ili kutambua gharama halisi wanazopaswa kulipa na kuepuka kubambikiziwa bili zenye gharama kubwa kutokana na uwepo wa baadhi ya wasoma mita wasio waaminifu.

Maelekezo hayo yametolewa wilayani Chamwino mkoani Dodoma na naibu waziri wa maji Jumaa Aweso katika ziara ya kukagua miradi ya maji ambapo ameagiza wakurugenzi wote wa mamlaka za maji nchini kutoa muongozo kwa wasoma mita pindi wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao wahakikishe wanawashirikisha watumiaji wa maji ili kudhibiti ubambikizwaji wa bili.

Naibu waziri Aweso amelazimika kutoa maelekezo hayo baada ya kubaini kuwa wengi wa watumiaji wa huduma ya maji hawana uelewa wa namna ya kusoma mita zao na kutambua bili wanazopaswa kulipa.

Post a Comment

0 Comments