tangazo

Waziri jafo amwagia sifa DC Jokate ''wewe unapiga kazi na shule hii itaitwa Jokate''

Waziri wa Tamisemi Sulemani Jafo ameagiza kuanza kwa ujenzi mpya wa shule ya Sekondari Kisarawe pamoja na kuanza kufanya kazi kwa Zahanati ya Mhaga iliyopo Wilayani Kisarawe ili kupunguza changamoto za elimu na afya katika wilaya hiyo.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua shule iliyojengwa kupitia kampeni ya tokomeza zero chini ya mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ambapo amesema pa moja na kujengwa kwa shule ya Kisarawe na Zahanati pia anatarajia kuongeza madarasa, maabara na majengo mengine ili kukamilisha shule hiyo iliofikia asilimia 70.

Kwa upande wake DC Jokat amesema shule hiyo inakuwa ya 17 katika wilaya ya kisarawe ambapo mchakato wa waalimu pa moja na usajili umeshaanza hasa baada ya waziri kumpendekeza mwalimu mkuu wa shule hiyo ambayo imepewa jina Jokate Sekondari Mariam Mpunga ambaye awali alikuwa Mwl Wa shule ya Msingi Kibuta 

Post a Comment

0 Comments