Wito wa euro bilioni 8 watolewa na viongozi wa Umoja wa Ulaya

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na viongozi wengine wa Umoja wa Ulaya wameandika barua ya wazi, inayohimiza ufadhili mkubwa kwaajili ya upatikanaji wa chanjo na dawa za kutibu virusi vya corona.
Wito wao umekuja kuelekea mkutano wa mchango wa dunia utakaoandaliwa na Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jumatatu wiki ijayo, ukiwa na lengo la kuchangisha euro bilioni 7.5 zitakazotumika kufanyia utafiti wa utambuzi, matibabu na chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Viongozi hao wamesema katika barua hiyo iliyochapishwa leo katika gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung kuwa wataweka kiwango cha mchango wao mezani na kutarajia kuungwa mkono na washirika wengine duniani.

Baadhi ya washirika waliotia saini barua hiyo ni pamoja na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte, Waziri Mkuu wa Norway Erna Solberg, Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel na rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen

Post a Comment

0 Comments