ZFF watoa tamko ligi kurejea tena viwanjani

SHIRIKISHO  la Soka visiwa Zanzibar (ZFF), limesema kwamba lipo tayari kuendelea na ligi kuu na ligi za madaraja yote za  msimu wa  mwaka 2019-2020 uliolazimika kusimamishwa kufuatia kuenea kwa Virusi vya Corona (COVID 19) Nchini.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho hilo, Ali Mohamed Ali alisema kwamba ZFF imefikia hatua hiyo kutokana  na agizo walilopatiwa na Shirikisho la mpira wa mguu barani afrika CAF kuwa hadi ifikapo May 5 wawe wameshatoa hatma za ligi za msimu wa mwaka 2019/2020.


"Leo tushawajibu CAF kwa barua kuwa ligi zote za madaraja zitaendelea ikiwa hali itaruhusu, nafikiri ligi za Madaraja ya Vijana hazitoendelea tena, kwaiyo CAF tumewajibu ligi yetu imesimama ikiwa hali itaruhusu tutaendelea, hapa kubwa tunasubiri zuio la serikali tu, wakiruhusu shughuli ziendelee, na muda ikiwa upo tutacheza tu, alobakisha mechi 8 atacheza 8, alobakisha 5 atacheza 5". Ali Muhammed Mkurugenzi wa Mashindano ZFF.

Post a Comment

0 Comments