tangazo

George Floyd azikwa Texas karibu na kaburi la mama yake

George Floyd amezikwa leo jimboni Texas nchini Marekani wakati taifa hilo likimuaga Mmarekani huyo mweusi mwenye umri wa miaka 46 ambaye kifo chake wiki mbili zilizopita akiwa mikononi mwa polisi weupe kilizusha vuguvugu la kitaifa la kudai mageuzi.

 Mwili wa Floyd ulitolewa katika kanisa la Fountain of Praise katika mji alikozaliwa wa Houston, hadi makaburi yaliyo karibu ya Pearland, na kuzikwa katika hafla ya faragha iliyohudhuriwa na wanafamilia wake.

 Amezikwa karibu na kaburi la mama yake. Waombolezaji walijazana barabarani kwenye msafara, ambao ulijumuisha farasi weupe waliobeba jeneza lake katika mkondo wa mwisho wa safari yake.

Mapema jana mamia ya watu walioalikwa walihudhuria ibada ya mazishi mjini Houston. Miongoni mwa waliohudhuria ni watu mashuhuiri, wanasiasa, na familia za wamarekani wengine kadhaa weusi waliouawa mikononi mwa polisi kote nchini humo.

Waliozungumza katika hafla hiyo walishinikiza kupatikana haki dhidi ya chuki na ubaguzi wa rangi. Ibada hiyo ya mazishi ilionyeshwa moja kwa moja na vituo vyote vya televisheni nchini humo.

Post a Comment

0 Comments