Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 19.09.2023

tt

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mlinda mlango huyo wa Uingereza na Arsenal Aaron Ramsdale

Chelsea na Bayern Munich wanamfuatilia Aaron Ramsdale, 25, baada ya mlinda mlango huyo wa Uingereza na Arsenal kuachwa nje ya mechi ya The Gunners dhidi ya Everton siku ya Jumapili. (Daily Mail)

Manchester United inaandaa ofa ya kumnunua mshambuliaji wa Bayern Munich na Ujerumani Serge Gnabry huku klabu hiyo ikiwa tayari kutoa takriban pauni milioni 52 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Fichajes - kwa Kihispania)

Beki wa Atletico Madrid na Uruguay Jose Maria Gimenez, 28, pia anavutiwa na Manchester United. (FourFourTwo)

Newcastle wanafikiria kutoa ofa ya pauni milioni 52 kumnunua kiungo wa West Ham Lucas Paqueta. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alihusishwa na Manchester City msimu wa joto lakini uhamisho huo ulitibuka kufuatia uchunguzi wa madai ya ukiukaji wa kamari uliofanywa na Mbrazil huyo. (Daily Mail)

Lucas Paqueta

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa West Ham Lucas Paqueta

Mlinzi wa Uingereza Trent Alexander-Arnold anakaribia kufikia mkataba mpya na Liverpool licha ya Barcelona na Real Madrid kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (90min)

Kiungo wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 29, atagharimu klabu yake inayofuata pauni milioni 50 kutokana na mkataba wake mpya ikiwa ni pamoja na kipengele cha kutolewa. (Fabrizio Romano)

Beki wa Ufaransa Giulian Biancone, 23, amekamilisha uhamisho wa kudumu kutoka Nottingham Forest hadi Olympiacos. (The Athletic -Usajili unahitajika)

tt

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mchezaji wa Liverpool Montevideo Fabricio Diaz, 20, anahamia klabu ya Qatar Al Gharafa huku kiungo huyo wa Uruguay akivutiwa na Brighton na Barcelona. (Fabrizio Romano)

Kiungo wa kati wa Ujerumani Julian Draxler, 29, amejiunga na klabu ya Al Ahli SC ya Qatar kutoka Paris St-Germain kwa mkataba wa kudumu. (Fabrizio Romano)

Beki wa Chelsea mwenye umri wa miaka 19 Muingereza Alfie Gilchrist ameongeza mkataba wake wa mwaka mmoja hadi Juni 2025. (Standard). 

Chanzo: BBC Swahili

Post a Comment

0 Comments