Tetesi za soka Ulaya Jumapili 25.08.2019:

 Zaha, Neymar, Morrison, Sanchez, Gracia

Wilfried Zaha
PSG inapanga kuwasilisha dau la £100m ili kumnunua winga wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha 26 ili kuchukua mahala pake mshambuliaji wa Brazil Neymar 27.(Sunday Mirror)
Manchester United inafikiria kuwasilisha ombi la kumsajili kiungo wa kati wa Leicester City James Morisson mwezi Januari ambaye anadaiwa huenda akagharimu£80m. (Sunday Mirror)
Manchester United na Inter Milan zitaendelea na mazungumzo siku ya Jumatatu kuhusu makubaliano ya mkopo wa mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez. (Observer)
Alexi SanchezHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAlexi Sanchez
Watford inafikiria hatma ya mkufunzi wake Javi Gracia baada ya kuanza kampeni yao ya Premia baada ya kupoteza mara tatu na hivyobasi kushindwa mara saba mfululizo kutoka msimu uliopita.. (Mail on Sunday)
Real Madrid itawasilisha ombi la kumsaini kipa wa Everton mwenye umri wa miaka 36 Maarten Stekelenburg iwapo mlinda lango wao raia wa Chile Keylor Navas, 32, atahamia PSG. (Football Insider)
United itafikiria kumsaini kipa wa Croatia Dominik Livakovic, 24, kwa dau la £20m kutoka Dinamo Zagreb iwapo raia wa Uhispania David de Gea, 28, hatotia saini ya mkataba mpya katika uwanja wa Old Trafford. (Sun on Sunday)
David De Gea
Real Sociedad imekubali kumsaini beki wa Arsenal na Uhispania Nacho Monreal, 33. (Marca - in Spanish)
Tottenham wana matumaini kwamba beki wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 30 Toby Alderweireld atatia kandarasi mpya . (Sun on Sunday)
Fiorentina imejiunga katika harakati za kumsaini mshambuliaji wa Liverpool na Enlgand Bobby Duncan kwa mkataba wa msimu huu . (Mail on Sunday)
Pualo Dybala
Paris St-Germain inajaribu kutatua haki za mauzo za Paulo Dybala huku wakitaka kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Argentina kutoka Juventus.(Calciomercato)
Southampton inamchunguza mshambuliaji wa QPR mwenye umri wa miaka 21 Eberechi Eze kabla ya uhamisho wa mwezi Januari . (Sun on Sunday)
Sampdoria ina hamu ya kumsaini kipa wa Aston Villa na Croatia Lovre Kalinic, 29. (Il Secolo XIX - in Italian)
Fifa inachunguza iwapo Roboti zinaweza kuchukua mahala pao marefa wa usaidizi ili kutoa maamuzi ya mipira ya kuotea kwa kuwa tayari wanasaidia katika VAR. (Sunday Mirror)

TETESI JUMAMOSI

NeymarHaki miliki ya pichaAFP
Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali ya mchezaji huyo kujeruhiwa mara kwa mara. (Marca - in Spanish)
Lakini ripoti zinaarifu kuwa Real na mahsimu wao Barcelona wanahoji masharti ya malipo ya hali ya juu yanayodaiwa na Neymar. (AS - Spanish)
Baba mzazi wa na wakala wa beki wa Arsenal wa miaka 27-Shkodran Mustafi wanasema mchezaji huyo raia wa Ujerumani ana mpango wa kuhama klabu hiyo. (Mirror)
Mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk, 28, anatarajiwa kutia saini kandarasi mpya na klabu hiyo ambayo itaongeza mara mbili malipo ya mchezaji huto wa raia wa Uholanzi hadi £250,000 kwa wiki. (90min)
Alexis SanchezHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Chile, Alexis Sanchez
Manchester United wana matumaini ya kumuuza mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 30, kabla dirisha la usajili wa wachezaji barani ulaya kufungwa. (Mirror)
Wachezaji wa United wanataka mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 21, awe akipiga mikwaju ya penalti baada ya mkwaju wa penalti wa Paul Pogba kushikwa wakati wa mechi yao dhidi ya Wolves. (Mail)
Tottenham wanatafakari kumuuza kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27, wakipokea dau la angalau £50m. (Mail)
Christian EriksenHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDenmark Christian Eriksen, Kiungo wa kati wa Tottenham
Winga wa Manchester City Mjerumani Leroy Sane, 23, huenda akarejea uwanjani msimu huu baada ya kuumia goti wakati wa michuano ya Community Shield mapema mwezi Agosti. (Sun)
Bayern Munich wanajiandaa kujaza pengo lililoachwa na mchezaji wa kimataifa wa Ureno Renato Sanches,aliyejinga na Lille, kiungo wa kati wa Espanyol Mhispania Marc Roca anapigiwa upatu kuchukua nafasi hiyo. (L'Equipe - in French)
Keylor NavasHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKeylor Navas, Kipa wa Real Madrid
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane haamini kipa wake Keylor Navas, 32, ataondoka klabu hiyo licha ya tetesi zinazomhusisha na Paris St-Germain.(Marca)
Crystal Palace wanashauriana na mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 28 kuhusu mkataba mpya. (Evening Standard)
Tottenham huenda wakapata nafasi ya kumsajili mshambuliaji Paulo Dybala, 25, mwezi Januari ikiwa nyota huyo wa kimataifa wa Argentina atasalia Juventus. (Football.London)
Paulo DybalaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPaulo Dybala
Juve wanasemakana kuvutiwa na wazo la kiungo wa kati Miralem Pjanic, 29, raia wa Bosnia kuondoka klabu hiyo msimu huu wa uhamisho wa wachezaji.(calciomercato)

Tetesi Bora Ijumaa

Ujumbe wa wawakilishi wa Real Madrid upo Ufaransa kufanya majadiliano juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27 kutoka klabu ya Paris St-Germain. (Marca - in Spanish)
Barcelona wamekataa ofa ya klabu ya Inter Milan ambao wanataka kumsajili kiungo wa kimataifa wa Chile Arturo Vidal, 32, kwa mkopo. (Mundo Deportivo)
Arturo VidalHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionArturo Vidal
Mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 28, na mlinzi raia wa England James Tomkins, 30, wapo katika mazungumzo ya kuongeza mikataba yao na klabu ya Crystal Palace. (Guardian)
Winga raia wa Brazil anayekipiga na klabu ya Chelsea Kenedy, 23, anaangalia uwezekano wa kuihama moja kwa moja klabu hiyo kabla ya dirisha la usajili la ulaya kufungwa wiki ijayo. (Goal)
Miamba ya Uturuki klabu ya Fenerbahce imejitenga na harakati za uhamisho wa beki wa Manchester United na Argentina Marcos Rojo, 29. (Star)

Post a Comment

0 Comments