Australia: Rubani mwanagenzi atua ndege salama baada ya mwalimu kuzirai


Mwanafunzi alitua salama ndege aina ya Cessn (rubani hakupigwa picha)katika uwanja wa ndege wa Perth
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwanafunzi alitua salama na ndege aina ya Cessn (rubani hakupigwa picha)katika uwanja wa ndege wa Perth
Rubani mwanafunzi nchini Australia amefanikiwa kutua ndege salama baada ya mwalimu wake kuzirai akiwa mitamboni.
Max Sylvester, makazi wa Australia magharibi iliwasiliana kwa dharura na waelekezi wa ndege saa moja baada ya mwalimu wake kuzirai wakiwa angani siku ya Jumamosi.
Wahudumu hao walimsaidia mwanafunzi huyo kutua ndege salama katika uwanja wa ndege wa Perth.
Bw Sylvester alisifiwa kwa kuchukua hatua ya haraka na kuwa mtulivu wakati wa tukio hilo.
Katika mawasiliano yaliorekodiwa na baadae kuwekwa wazi kwa umma, Slivester alielezea hali ya mwalimu wake kabla ya kuchukua jukumu la kupaisha ndege hiyo.
"Ananitegemea bega lngu, Najaribu kumuamsha lakini anaanguka," aliwaambia mafundi wa mitambo.
Alipoulizwa kama anajua jinsi ya kupaisha ndege aina ya Cessna, alijibu: "Hili ni somo langu la kwanza".
Bw. Sylvester aliwahi kupata mafunzo ya kupaisha ndege angani mara mbili chini ya uelekezi wa mwalimu wake na ilikua ndege aina nyingine lakini haikuwahi kutua.
Baada ya kupaa juu ya uwanja wa ndege wa Perth kwa karibu saa moja akifuata maagizo ya jinsi ya kutua,hatimae alifanikiwa kutua salama ndege hiyo huku maafisa wa kukabiliana na hali ya dharura pamoja na familia yake wakimsubiri.
Mwalimu alipelekwa hospitali na ripoti zinasema kuwa anaendelea kupata nafuu.
"Ndege haikuharibika hata kidogo. Kusema kweli alitua kama rubani mzoefu," alisema Chuck McElwee, mmiliki wa chuo cha urubani.
Alimsifu mwanafunzi na waelekezi wa ndege akisema: "Sio rahisi kupata ushirikiano kama huo mara kwa mara."

Post a Comment

0 Comments