tangazo

Chicharito atua Sevila


Mshambuliaji Javier Hernandez maarufu kama Chicharito ametangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Klabu ya Sevilla ya Hispania akisaini mkataba wa miaka mitatu akitokea West Ham United.

Hernandez raia wa Mexico mwenye umri wa miaka 31 ametambulishwa leo akiwa kwenye Uwanja wa Sevilla, Sanchez Pijuan nchini Hispania lakini kiasi cha ada ya uhamisho hakijawekwa wazi.

Mshambuliaji huyo anaondoka West Ham United akiwa ameitumikia kwa muda wa miaka miwili ikiwa katika Ligi Kuu ya England akiwa ameichezea mechi 55 na kufunga mabao 16 likiwemo moja alilofunga msimu huu katika sare ya bao 1-1 dhidi ya Brighton.

Post a Comment

0 Comments