tangazo

Chuo Kikuu cha Zimbabwe kimeahirisha Mahafali kufuatia kifo cha Mugabe


Chuo Kikuu cha Zimbabwe kimeahirisha hafla ya kuhitimu ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika  Septemba 14 na wiki moja kufuatia kifo cha rais wa zamani Robert Mugabe.

Katika taarifa kwa waandishi wa habari iliyotolewa Jumanne na idara ya habari na uhusiano wa umma, chuo kikuu kinachoongoza nchini kimesema kuwa sherehe ya kuhitimu sasa itafanyika Septemba 20 mwaka huu.

Serikali tayari imetangaza kuwa Mugabe, aliyefariki akiwa nchini Singapore mnamo Septemba 6, atazikwa siku ya Jumapili, Septemba 15, ingawa haikuonyesha ni wapi mazishi hayo yatafanyika.

Kumekuwa na ripoti kwamba Mugabe, ambaye alijiuzulu kama Rais mnamo Novemba 2017, alikuwa amesema kuwa hataki kuzikwa kwenye "National Heroes Acre" mjini Harare.

Familia yake bado haijathibitisha tarehe ya mazishi na msemaji wa familia Leo Mugabe aliwaambia wanahabari kwamba viongozi wa jadi katika kijiji cha Zvimba ambako nyumbani kwa Mugabe watatangaza juu ya suala hilo

Post a Comment

0 Comments