Virusi vya corona: Senegal yakanusha kuagiza dawa ya mitishamba kutoka Madagascar

 Rais Rajoelina ametaka wanafunzi wapewe kinywaji hicho kwa kiwango kidogo kila baada ya muda kwa siku.
Senegali imekanusha madai kwamba imeagiza kile ambacho kinasemekana ni dawa ya virusi vya corona ambayo inapigiwa upatu na Rais wa Madagascar Andry Rajoelina, shirika la habari la RFI limeripoti.
Wiki jana, Shirika la Afya Dunia (WHO) lilisema hakuna ushahidi unaoonesha kwamba dawa hiyo ni tiba ya ugonjwa wa Covid-19 baada ya Rais kuizindua rasmi dawa hiyo ya mitishamba inayotengenezwa Madagascar.
Dawa hiyo iliyo kwenye chupa na chai za mitishamba vimekuwa vikinadiwa na rais baada ya kufanyiwa majaribio kwa zaidi ya watu 20 katika kipindi cha wiki tatu, mkuu wa wafanyakazi Lova Hasinirina Ranoromaro aliliambia shirika la BBC.
Ijumaa, Rais Rajoelina aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter, kwamba rais wa Senegal Macky Sall, ameagiza dawa hiyo.
Lakini chanzo kilichonukuliwa na RFI kimesema kwamba hakuna oda kama hiyo iliyoagizwa.
Bwana Sall ameandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kwamba nchi yake inafuatilia utafiti huo kwa karibu.
Rais Rajoelina pia naye ameandika ujumbe kwamba rais wa Guinea-Bissau ametuma ndege tayari kuchukua dawa hiyo ya mitishamba aliyoagiza.

Kujibu uzinduzi wa dawa hiyo, WHO ilisema kwenye taarifa iliyotumwa kwa BBC, kwamba shirika hilo halipendekezi kujitibu kwa kutumia dawa yoyote... kama njia moja ya kuzuia au tiba ya ugonjwa wa Covid-19.
Shirika hilo lilirejelela matamshi ya Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Adhanom Ghebreyesus kwamba hakuna mkato katika kutafuta tiba ya uhakika ya kupambana na virusi vya corona.
Majaribio katika ngazi ya kimataifa yanaendelea kutafuta tiba stahiki ya kukabiliaba na virusi hivi, WHO iliongeza.

Post a Comment

0 Comments