tangazo

Clouds yatoa mavazi maalum kwa wauguzi seti 100 kwaajili ya mapambano ya corona

CEO wa Clouds Media Group Joseph Kusaga wakati akizindua kampeni ya 'Bonge la MPAMBANAJI' leo amesema kwamba CLOUDS inatoa full set ya Mavazi maalum ya kujikinga (PPE) 100 kusaidia Wauguzi.

“Sio kila kitu cha kumuachia Rais hasa kwenye mapambano haya ya corona, yoyote ambaye anaweza kutoa chochote anaruhusiwa na mimi nimejitolea kutoa full set za PPE 100 kwa wauguzi wetu”

“Wahudumu wa Afya ni Watu wanaojitoa kukupima wewe, hawajui kama una corona au hauna na huyo Mtu amejitoa maisha yake kwa kukusaidia wewe maisha yako na huku akijua kama atapona au ataambukizwa, kila kitu sio cha kumuachia Rais peke yake”-KUSAGA

Post a Comment

0 Comments