tangazo

Kikosi cha Simba chaanza mazoezi ndani ya Mo Arena

Kikosi cha Simba leo kimetia timu katika uwanja wa Mo Arena kuanza kufanya mazoezi kwa ajili kuanza maandalizi kuelekea kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.

Wachezaji wa Simba wameripoti leo kambini na kufanyiwa vipimo vya afya pamoja na maelekezo mengine kuhusu kujilinda na Virusi vya Corona.

Leo inakuwa ni mara ya kwanza kwa wachezaji wa Simba kufanya mazoezi kwa pamoja baada ya masuala ya michezo kusimamishwa Machi 17 na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Baadhi ya nyota ambao wamewasili ni pamoja na Pascal Wawa, Jonas Mkude, Meddie Kagere, Gadiel Michael, Shomari Kapombe, Aish Manula na Tairone Santos.

Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuanza Juni Mosi.

Post a Comment

0 Comments