Kubadilika umbo kwa virusi vya corona: Fumbo kwa wanasayansi juu ya athari za virusi

Watafiti wamekua wakifuatilia mabadiliko hadi ' tawi ' linalochomoza la kirusi

Watafiti nchini Marekani na Uingereza watambua mamia ya mabadiliko ya maumbile ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Lakini hakuna hata mmoja ambaye amefahamu ambacho hii itamaanisha katika kusambaa kwa virusi miongoni mwa watu na ikiwa chanjo itakua na ufanisi.

Virusi vinabadilika maumbile-hicho ndicho kinachotokea.

Tatizo ni: aina gani ya maumbile haya yanayoleta mabadiliko ya kuufanya ugonjwa uwe mbaya zaidi au kuyafanya maambukizi kuwa ugonjwa?

Utafiti wa awali kutoka Marekani umeelezea kuhusu moja ya mabadiliko ya kimaumbile uliouita - D614G - ambayo yamejitokeza zaidi na huenda kukasababisha maambukizi makali zaidi.

Hatahivyo bado haujatathminiwa na wanasayansi wengine na kuchapishwa rasmi.

Watafiti, kutoka Maabara ya Los Alamos National Laboratory nchini New Mexico, wamekua wakifuatilia mabadiliko hadi kufikia "tawi" la kirusi yanayoleta mabadiliko ya kipekee ya kimaumbile, kwa kutumia mfumo wa data uliopangwa unaoitwa Global Initiative on Sharing All Influenza Data (GISAID).

Walibaini kuwa inaelekea kuna kitu fulani kuhusu mabadiliko hayo ya kimaumbile yanayokifanya kirusi kukua haraka zaidi - lakini athari za mabadiliko haya bado hazijawa wazi.

Timu ya utafiti iliyotathmini data za Uingereza kutoka kwa wagonjwa wa virusi vya corona katika eneo la Sheffield. Ingawa walibaini kuwa watu wenye virusi hivyo vinavyobadilika umbo walionekana kuwa na kiwango kikubwa cha virusi katika sampuli zao za vipimo, hawakupata ushahidi wa wazi kwamba watu wale waliugua au walilazwa hospitalini kwa muda mrefu.

'Kubadilika kwa maumbile sio jambo baya'

Utafiti mwingine kutoka taasisi ya Chuo Kikuu cha London-University College London n(UCL) ulibaini virusi sampuli 198 zilizokua na mabadiliko ya kimaumbile ya virusi yanayorudia.

Mmoja wa waandishi wa utafiti huo, Profesa Francois Balloux, alisema: "Mabadiliko ya maumbile yenyewe sio kitu kibaya na hakuna kutu chochote kinachoonyesha kuwa kirusi cha SARS-CoV-2 kinabadilika kimaumbile haraka au polepole kuliko inavyotarajiwa.

"Hadi sasa hatuwezi kusema iwapo SARS-CoV-2 vinakua na makali zaidi au kidogo au vinaambukiza zaidi"

Utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Glasglow ambao pia ulitathmini mabadiliko ya kimaumbile ya virusi vya corona, ulisema kuwa mabadiliko haya hayasababishi aina nyingine ya virusi. Walisema kuwa ni aina moja tu ya virusi ambayo kwa sasa inazunguka.

Kufuatilia mabadiliko madogo kwenye muundo wa virusi ni muhimu katika kuelewa maendeleo ya chanjo.

Mfano ukiangalia 'virusi vya mafua: hubadilika haraka sana kiasi kwamba inalazimika kufanyia mabadiliko chanjo yake kila mwaka ili kukabiliana na aina fulani ya mafua yanayoenea.

Utengenezaji wa dawa

Nyingi kati ya chanjo za Covid-19 kwa sasa zinaendelea kutengenezwa, kulenga aina fulani ya virusi-wazo ni kulenga mwili wako utambue aina ya kipekee ya tawi la kirusi ambayo itasaidia kupambana na kirusi kizima. Lakini kama tawi hilo linabadilika, chanjo inayotengenezwa kwa njia hii inaweza kuwa na ufanisi mdogo.

Kwa sasa yote haya ni nadhar ia. Wanasayansi bado hawajapata taarifa za kutosha kusema ni mabadiliko gani yanayotokea kwa kirusi na yata maanisha nini.

Dkt Lucy van Dorp, mtafiti mwenza katika taasisi ya London-University College London, alisema kuwa na uwezo wa kutathmini idadi kubwa ya mabadiliko ya seli za urithi za kirusi huenda "kusiwe na thamani katika juhudi za utengenezaji wa dawa ".

Hata hivyo ameiambia BBC : "Ninapenda kutathmini seli za urithi, lakini kuna mengi sana wanayoweza kusema."

Unaweza pia kutazama:

Ni lini Chanjo ya corona itapatikana?

Post a Comment

0 Comments