tangazo

McConnell amtaka Obama afunge mdomo wake badala ya kumkosoa Trump kuhusiana na corona

Kiongozi wa Warepublican waliowengi katika Seneti ya Marekani amesema, ingepasa rais wa zamani Barack Obama afumbe mdomo wake badala ya kukosoa utendaji wa rais wa nchi hiyo Donald Trump kuhusiana na janga la corona.

Mitch McConnell amesema, ingefaa Obama afuate desturi ya rais aliyemtangulia George W, Bush ambaye alijitenga na siasa kwa kiasi kikubwa baada ya kuondoka Ikulu ya White House.

McConnell ameongeza kuwa: "Nafikiri ingepasa Obama afumbe mdomo wake. Tunajua hapendezwi hata kidogo na kazi zinazofanywa na serikali hii. Tunaweza kumuelewa, lakini hailaiki kukosoa serikali iliyokuja baada yako."


Hivi karibuni, Obama alitoa matamshi makali ya kukosoa utendaji wa Trump katika kukabiliana na janga la Corona akiuelezea kuwa ni "janga kamili la machafuko".  Obama alitoa matamshi hayo katika mazungumzo na wafanyakazi wake wa zamani kuungana na timu ya kampeni ya uchaguzi ya aliyekuwa makamu wake wa rais Joe Biden, anayetazamiwa kuchuana na Trump katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais wa Marekani utakaofanyika Novemba mwaka huu.

Hayo yanajiri huku takwimu zikionyesha kuw,a hivi sasa Marekani ina jumla ya watu 1,385,834 waliokumbwa na ugonjwa wa Covid-19, ambapo 81,795 miongoni wao wameshafariki dunia kwa ugonjwa huo na kuifanya nchi hiyo muathirika mkubwa zaidi wa janga la virusi ya corona duniani.

ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments