Mchezaji wa Coastal Union Bakari Mwamnyeto kutua Simba SC

BAADA ya kuwepo kwa tetesi nyingi juu ya beki wa kati wa Coastal Union ya Tanga, Bakari Mwamnyeto kutakiwa na Simba, hatimaye uongozi wa Klabu ya Simba umeweka wazi juu ya suala hilo

Simba kupitia ofisi ya mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mazingisa inadaiwa kuwa imesema kuwa ni kweli mchezaji huyo inamuhitaji na tayari umeshampatia ofa yake ili aweze kujiunga na timu hiyo.

Akizungumza na  mmoja wa viongozi wa Simba kutoka ndani ya ofisi hiyo ya Senzo alisema kuwa uongozi huo upo tayari kutoa kitita cha Sh milioni 80 ili kumsajili mchezaji huyo.

Mtoa taarifa huyo ameeleza kuwa Sh milioni 50 ni kwa ajili ya Mwamnyeto mwenyewe na Sh milioni 30 ni kwa ajili klabu yake ya Costal Unioni kama ada ya uhamisho wake kwa kuwa bado ana mkataba.

“Ofa hiyo tulimpatia tangu dirisha dogo la usajili lakini akaikataa kuwa ni kidogo anataka yeye peke yake achukue Sh milioni 80 zote.

“Jambo hilo uongozi haukukubaliana nalo na ukaamua kuliacha kama lilivyo, kwa hiyo kama atakubali kuchukua kiasi hicho basi atasajiliwa kama hakikataa basi akatafute timu nyingine,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipotafutwa Senzo ili azungumzie hilo hakupatikana lakini kwa upande wake, Mwamnyeto yeye hakutaka kusema chochote kuhusiana na hilo

Post a Comment

0 Comments