tangazo

"Sisemi uongo raundi hii nikijua naua mtu"-Shilole

Msanii na mfanyabiashara maarufu hapa nchini Shilole, ametoa onyo kwa mwanamke yeyote ambaye atamkuta na mume wake Uchebe kwa kusema ataua mtu.

Ameeleza hayo kwenye show ya Planet Bongo ya East Africa Radio, wakati akitambulisha wimbo wake mpya na kusema cha msingi ni kuvumiliana kwenye shida na raha, ila endapo akijua kama ana mwanamke mwingine ataua na kila abiria achunge mzigo wake.

"Tutatafutana Jerusalem sisemi uongo na raundi hii nikijua naua Magufuli atakuja kunitoa, sina asilimia 100 kama ananisaliti au hanisaliti kwa sababu yule ni mwanaume kama wanaume wengine, kama anafanya mambo yake afanye ila mimi nisijue, kwani nani asiyejua kwamba Shilole mumewe ni Uchebe, halafu ndiyo nikukute naye sijui utaniambia nini nakupasua koromeo, abiria chunga mzigo wako" ameeleza Shilole.

Post a Comment

0 Comments