tangazo

Rais Dr. John Magufuri awahakikishia Walimu na Wafanyakazi wote mishahara yao Hata wakati huu wa Janga la Corona

Watanzania Wamshukuru MUNGU kwa uongozi huu wa serikari ya Rais John Magufuri. Rais ambaye anauchungu na raia mmoja mmoja hata zaidi ya mwanae wakumzaa, Rais anaeguswa na maumivu ya raia wake nakuchukua hatua.

Rais Magufuri katika hotuba yake Jana Tarehe 04/05/2020 amewahakikishia Wafanyakazi wote kuendelea kulipwa mishahara yao, hata walimu ambao wapo nyumbani kutokana na janga hili bado watalipwa mishahara yao yote.

Ni wito wetu raia Watanzania kuzidi kumuunga Rais wetu juhudi nakuzidi kumuombea kwa MUNGU. Aidha juhudi za kujenga uchumi zizidi kushika kasi zaidi ili tulijenge Taifa letu liwe nanguvu ili tupite salama katika janga hili.
Wakulima kaza jembe, Wafanyakazi na nawafanya biashara ongezeni ubunifu nauchapakazi wa halo ya juu. MUNGU ibariki Tanzania, MUNGU mbariki Rais wetu John Magufuri.

 Na  Joshua Vedasto. W

Tazama Video ya kipande cha hotuba ya Rais hapa Usisahau Ku subscribe


Post a Comment

0 Comments