tangazo

Ujerumani yasisitiza mshikamano na NATO

Ujerumani imesema silaha za nyuklia za Marekani ambazo pia zimewekwa nchini Ujerumani ni sehemu ya ulinzi. Ujerumani imeleeza kwamba itaendelea kutoa mchango wake katika mkakati wa ulinzi wa kinyuklia kwenye mfungamano wa kijeshi wa NATO.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani ametoa tamko hilo baada ya wanachama waandamizi wa chama cha Social Demokratic SPD kutoa wito wa kuondolewa kwa silaha hizo za Marekani zilizowekwa hapa nchini Ujerumani.

 Chama hicho cha SPD kimo katika serikali ya mseto inayoongozwa na kansela Angela Merkel. Marekani imeweka makombora ya nyuklia yapatayo 150 katika nchi kadhaa za Ulaya ikiwa pamoja na Ujerumani

Post a Comment

0 Comments