Virusi vya corona: Wagonjwa ambao dalili za Covid-19 haziishi haraka

David huwasiliana na familia yake kupitia dirisha

Maisha ya David Harris yalisalia kuwa ya chumba chake na mahali alipoweza kufika ni hadi mlango wa mbele wa chumba chake.

Wiki saba zilizopita alipata dalili za Covid-19 ambazo anazielezea kuwa zilikua zinafanana na za mafua makali.

Hapo ni wakati mhandisi huyo wa umri wa miaka 42, alipoanza kujitenga mwenyewe nyumbani kwake katika mji wa Bristol ambamo alikua akiishi na mke wake pamoja na mtoto wake mchanga wa kike.

Na baada ya wiki au zaidi alianza kujihisi vizuri, lakini wiki mbili baadaye dalili zake zikarejea tena, jambo lililomshangaza.

"Imekua ni kama wimbi la dalili linalorejea baada ya muda jambo ambalo sikuwa ninalitarajia kabisa," anasema.

" Wimbi la pili za dalili lilikua ni baya sana - dalili tu sawa na za mafua, lakini pia na kushindwa kupumua, na ndio maana nilikua ninaamini ni virusi vya corona.

"Halafu kulikua na wiki mbili ambapo nilidhani ninahisi vizuri sana, nilikua tu nimechoka sana.

"Halafu katika wiki ya saba, dalili zikaibuka tena na wimbi langu la tatu, kwa bahati nzuri sana dalili zilikuwa si kali sana lakini zilikuwepo ."

Kufanyia kazi nyumbani lilikua ni jambo jema, David aliendelea kujitenga mwenyewe, akibadilisha nguo na kuvaa nguo safi wakati nadra sana alipoondoka kupitia mlango wa chumba chake kuelekea bafuni, na kula na kulala peke yake.

Mke wake alikua akimleta mtoto wao mchanga wa kike mwenye miezi 10 Millie kwenye dirisha la chumba cha mbele ili David aweze kumuona kupitia dirisha la kioo.

Ugonjwa ulimdhoofisha David huku asijue ni nini kitakachomtokea.

"Huenda moja ya mambo yaliyomtia hofu zaidi ni kujaribu kuelewa ni katika hatua gani unaweza kuomba msaada wa kimatibabu

"Hutaki kuwasumbua wahudumu wa afya, kwasababu kuna watu kwa vyovyote vile walio katika hali mbaya zaidi yangu ''.

"Lakini hatimae sikutaka kuingia katika mtego wa kutoomba msaada halafu kitu kibaya kinitokee kwasababu haukuomba msaada.

"Dalili ziliponirudia, wakati nilipokuwa na hali mbaya sana, ni uzoefu unaotisha sana kwasababu haujui kama hiyo inamaanisha ndio unakuwa mahututi, mahututi, mahututi.

"Kwahivyo inatisha sana kuingia katika hali mbaya ya ugonjwa wakati unafikiria kwamba ulikua unaelekea kupona ."

Kuumia sana kimwili na kiakili

Felicity, mwenye umri wa miaka 49, kutoka London, ameingia wiki ya sita ya kupona baada ya kuugua aina ya dalili za Covid-19.

Lakini sawa na David, uzoefu wake haukuwa mzuri zaidi.

"Ninadhani sehemu ngumu zaidi ilikua ni kupitia siku 10 za mwanzo za kuumwa sana na nikafikiria ninaelekea kupona, mambo yakawa magumu na mabaya sana tena.

Felicity
Image captionFelicity alikua na dalili za corona kwa wiki sita

"Kwahiyo ilikua ni wiki yangu ya tano ya kuwa mgonjwa nikaomba msaada kwa kituo cha usaidizi wa taarifa za corona -A&E kwasababu nilikua ninahisi maumivu makali ya kutisha ya tumbo.

"Ni vigumu sana kujua ikiwa dalili ni za virusi? ni mfumo wa kinga unakabiliana? Ni maumivu gani yanaendelea ?

"Sikua na matatizo tumboni mwangu kabla ya kuugua, lakini wiki ya tano zilikuwa za maumivu makubwa sana."

Iwe Felicity au David wote hakuna ambaye amepimwa Covid-19, lakini wote waliambiwa na madaktari kuwa huenda walikua na virusi.

Pia wamehakikishiwa kuwa sasa hawana maambukizi.

Lakini Felicity alihangaika kupona dalili na wiki za kuumwa zimewaacha dhaifu.

"Ninatumia muda wangu mwingi chumbani kujaribu kupona.

"Uzoefu huu wote, wa kuwa mgonjwa na kujaribu kupona, umenichosha kiakili."

Virusi vya corona

Wengi hupona haraka

Sehemu ya tatizo ni kwamba mengi kuhusu virusi vya corona hayafahamiki, mkiwemo uzoefu wa baadhi ya watu wanaoopata dalili ambazo si kali sana na zinazodumu kwa siku chache, huku wengine wenye afya nzuri wakihangaika kwa siku kadhaa.

Dr Philip Gothard, Daktari katika hospitali ya majonjwa ya maeneo ya joto, anasema wengi miongoni mwa wagonjwa hupona kabisa kwa haraka.

"Baadhi wamekua wakiendelea kuwa na kikohozi na tumeanza kuona wagonjwa ambao huwa na uchovu mkubwa wa mwili ambao huendelea labda kwa wiku tatu, nne, tano au sita.

Inachosha sana kiakili hasa unapokua ni mtu mwenye umri mdogo na mwenye afya, kama hujazowea kuugua"

"Na kwahiyo inakuja kama mshituko kwamba kupona kunakua taratibu na kunako jirudia jirudia

"Lakini katika wagonjwa wengi wenye magonjwa mengine wanaopona baada ya ugonjwa mbaya hauoni aina hii ya dalili ambazo haziisha na athari zinazochosha wakati ukiendelea kupona, na kuwa na siku nzuri na mbaya ."

Tim Spector, profesa wa maradhi ya jeni katika King College London, anasema data zilizojitokeza kutoka katika utafiti wa dalili za Covid zinaonyesha kuwa, kwa wastani, huwachukua watu siku 12 kuanza kupona taratibu.

"Pia tunashuhudia idadi kubwa ya watu wanaoripoti dalili ambazo zinaweza kuendelea kwa muda mrefu zaidi kuliko hizi, baadhi yao hata siku 30 au zaidi.

"Huku tukikusanya data zaidi na kuendelea kutumia mashine kujifunza na akili bandia, hivi karibuni tutaweza kubaini ni mchanganyiko gani wa dalili na hatari vinavyoweza kumfanya mtu kuugua kutokana na dalili hizi za muda mrefu za virusi vya corona."

David na Felicity kwa pamoja wanatumai kuwa hatimae sasa wanapona na wanaweza kurejea katika maisha yao ya kawaida.

Lakini Covid-19, ugonjwa ambao umekuwepo kwa miezi kadhaa tu, unaendelea kutuonyesha maajabu.

Post a Comment

0 Comments