tangazo

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 23.06.2020: Jimenez, Martinez, Kurzawa, Arteta, Koulibaly, Vertonghen

Mshambuliaji wa Inter Milan, Lautaro Martinez
Barcelona imehusishwa na usajili wa mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez 22 lakini afisa mkuu mtendaji wa klabu hiyo Giuseppe Marotta anasema kwamba mchezaji huyo wa Argentina hajakuwa na hamu ya kutaka kuondoka ". (Sky Sports Italia, via Mail)
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta huenda akafikiria uhamisho wa bila malipo wa kipa wa England Joe Hart 33 , ambaye ataachiliwa na Burnley mwisho wa mwezi baada ya kipa wa Ujerumani Bernd Leno,28 kupata jeraha dhidi ya klabu ya Brighton. (Express)
Matumaini ya klabu ya Leeds United ya kumsaini kipa wa Argentina Emiliano Martinez, 27, kutoka Arsenal huenda yameambulia patupu kufuatia jeraha la Leno. (Express)
Emiliano MartinezHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKipa wa Argentina Emiliano Martinez, 27, kutoka Arsenal amejeruhiwa
Aliyekuwa mchezaji wa Brazil Ronaldo anasema kwamba klabu ya Real Valladolid itamkaribisha mchezaji wa Chile Alexis Sanchez iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 hatafanikiwa katika klabu ya Inter Milan, ambapo anahudumu kwa mkopo kutoka Manchester United. (Mirror)
Roma inaweza kuongeza kandarasi ya mkopo ya beki wa England Chris Smalling kutoka klabu ya Man United kwa msimu mwengine - kukiwa na chaguo la kumnunua kabisa mwisho wa kandarasi hiyo - huku mazungumzo yakiendelea kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 . (Tele Radio Stereo, via Football Italia)
Layvin KurzawaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionChelsea inamnyatia beki wa kushoto wa Ufaransa na PSG Layvin Kurzawa
Chelsea huenda ikaelekeza hamu yake ya kumsajili beki wa kushoto wa Ufaransa na PSG Layvin Kurzawa, 27 iwapo watashindwa kumsaini mchezaji wa leicester na England Ben Chilwell, 23 (Express)
Liverpool wamewasilisha dau la £54m kumsajili beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 pia anazivutia klabu za Manchester United na Chelsea. (Corriere dello Sport)
Kalidou KoulibalyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLiverpool wamewasilisha dau la £54m kumsajili beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly
Juventus iko tayari kuipatia wachezaji wawili wa Itali - beki Daniele Rugani, 25 na winga Federico Bernardeschi, 26 - klabu ya Wolves katika jaribio la kupunguza gharama ya kumnunua mshambuliaji wa Mexico Raul Jimenez, 29. (Tuttosport)
Roma imempatia beki wa ubelgiji Jan Vertonghen, 33, kandarasi ya miaka miwili huku kukiwa na chaguo la msimu wa tatu. (Il Messaggero, via Mail)
Klabu ya Uturuki ya Fenerbahce inapanga kuchangisha fedha kupitia mashabiki wake ili kuisaidia kumsajili kiungo mchezeshaji na mchezaji wa zamani wa Ujerumani Mesut Ozil 31 kutoka Arsenal. (Fotospor, via Star)
Mlinzi wa Tottenham Mbelgiji Jan VertonghenHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMlinzi wa Tottenham Mbelgiji Jan Vertonghen
Everton imejiunga katika kinyanganyiro cha kumsaini beki wa Real Valladolid Mohammed Salisu, 21. Raia huyo wa Ghana ambaye ana kifungo cha kumuachilia cha thamani ya £10.8m katika kandarasi yake pia anavutia Southampton na Manchester United. (Mail)
Kiungo wa kati wa Everton na Ufaransa Morgan Schneiderlin, 30, anatarajiwa kuondoka Goodison Park baada ya kupita vipimo vya afya katika klabu ya Ligue 1 nchini Ufaransa Nice. (Sky Sports)

Post a Comment

0 Comments