tangazo

Israel inasema kwamba ilishambulia maeneo ya ndege zisizo na rubani za Iran nchini Syria


Iran haina kinga kokote. alisema waziri mkuu wa Israeli Benjamin NetanyahuHaki miliki ya pichaAFP
Image captionIran haina kinga kokote. alisema waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Israel imeshambulia kambi za kijeshi za Iran nchini Syria ili kuzuia kile ilichokitaja kuwa utumizi wa ndege zisizokuwa na rubani kuishambulia.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alipongeza juhudi za operesheni hiyo iliotekelezwa na jeshi lake.
Israel inaaminika kutekeleza mamia ya mashambulio nchini Syria tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe 2011 ili kujaribu kuizuia Iran.
Msemaji wa jeshi la Israel alisema kwamba mashambulio hayo siku ya Jumamosi yalilenga wapiganaji wa Kikurdi wa Iran katika eneo la Aqraba , kusini mashariki mwa mji mkuu wa Damascus.
Duru za kjeshi za Syria zilizonukuliwa na chombo cha habari cha kitaifa cha Sanaa zilisema kwamba mifumo ya ulinzi ya angani ya Syria iligundua kwamba Israel ilikuwa inajiandaa kutekeleza mashambulizi kutoka katika milima ya Golan ikielekea katika mji wa Damascus.
''Uchokozi huo ulikabiliwa na kufikia sasa idadi kubwa ya silaha za Israel zimeharibiwa kabla ya kutimiza lengo lake'', duru hizo zilisema.
Katika ujumbe wa Twitter, Bwana Netanyahu alisema: Iran haina kinga kokote. ''Jeshi letu litatekeleza operesheni zake dhidi ya uchokozi wa Iran. Iwapo mtu anapanga kukuua muue wewe kwanza''.

'Shambulio la wazi'

Kwengineko ripoti zimesema kwamba ndege zisizo na rubani za Israel ambazo zilikuwa zikifanya uchunguzi ziliwasili katika ngome ya kundi la Hezbollah katika mji mkuu wa Lebanon wa Beirut.
Maafisa wa Hezbollah wamesema kwamba ndege zisizokuwa na rubani zilianguka katika paa ya kituo kimoja cha habari kinachomilikiwa na kundi hilo na ilifuatiwa na ndege nyengine isiokuwa na rubani ambayo ililipuka angani na kuanguka karibu na kitu hicho.

Hezbollah ilitoa picha za ndege moja ya rubaini ya israel iliolipukaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionHezbollah ilitoa picha za ndege moja ya rubaini ya israel iliolipuka

Wakaazi waliambia chombo cha habari cha AP kwamba walisikia mlipuko mkubwa ambao uliyumbisha eneo hilo baada ya kusikia sauti ya ndege
Jeshi la Israel lilikana kuzungumzia kuhusu ripoti hizo.
Waziri mkuu wa Lebanon Saad Hariri alitaja hatua hiyo ya Israel kama shambulio la wazi dhidi ya taifa huru la Lebanon.
''Uchokozi huu mpya ndio unaozua hofu ya usalama wa eneo hili lote na jaribio la kuzua hofu zaidi'' , alisema katika taarifa.
Israel pia ilidaiwa kutekeleza shambulio la angani mwezi uliopita katika hifadhi moja ya silaha nchini Iraq.
Gazeti la New York Times , lilinukuu maafisa wa Marekani ambao hawakutaka kujulikana wakisema kwamba ndio iliotekeleza shambulio la Julai 19 katika hifadhi ya silaha ambayo maafisa walikuwa wakisema kwamba inatumiwa na Iran kupeleka silaha Syria.
Jeshi la Israel limekataa kutoa tamko kuhusu shambulio hilo. .

Post a Comment

0 Comments