Ndege ya Air Tanzania yaachiwa Afrika Kusini Kwakishindo. Mafuriko Hayazuiwi kwa Mkono

Air Tanzania

Mahakama Kuu ya jimbo la Gauteng imeamuru ndege ya Air Tanzania iliyokuwa ikishikiliwa nchini Afrika Kusini kuachiwa mara moja.
Mwandishi wetu wa Afrika Kusini Nomsa Maseko anasema kuwa michakato ya kuichilia ndege hiyo kurejuea Dar es Salaam ikitokea katika uwanja wa ndege wa OR Tambo jijini Johannesburg inaendelea.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Damas Ndumbaro aliyekuwepo mahakamani ameileza BBC kuwa Tanzaia imeridhishwa na uamuzi wa mahakama.
Mkulima ambaye alipeleka shauri hilo mahakamani Hermanus Steyn na kupata kibali cha kushikiliwa ndege hiyo, Hermanus Steyn hajaridhishwa na hukumu.
Mwandishi wa BBC Maseko anaripoti kuwa Bw Steyn amekata rufaa, na shauri hilo linatarajiwa kuanza kusikilizwa leo hii.
Jaji TwalaHaki miliki ya pichaNOMSA MASEKO/BBC
Image captionJaji Twala M L akisoma hukumu yake mapema leo na kuamuru ndege ya Tanzania kuachiwa
Wakili wa Steyn ameileza BBC kuwa: "Tumearifiwa kuwa ACSA (kampuni inayoendesha viwanja vya ndege Afrika Kusini (ACSA) ipo katika harakati za kuiachia ndege. Kama ndege itaondoka Afrika Kusini, mteja wangu atapoteza bima yake, na jambo hili (rufaa) linahitaji kusikilizwa kwa haraka."
Dkt Ndumbaro ambaye pia ni wakili amesema kama Steyn bado ana malalamishi yeyote, inafaa arudi kwenye mahakama za Tanzania na kusikilizwa.
"Oh, niamini, raisi (John Magufuli) tayari ameshapewa taarifa (ya hukumu)," mwandishi wa BBC aliyepo mahakamani anamnukuu DkT Ndumbaro akisema.

Post a Comment

0 Comments