tangazo

Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 14.09.2019:

Mbappe, De Gea, Eriksen, Haller, Zaha

Kylina Mbappe
Barcelona huenda ikamsajili mshambuliaji wa PSG na Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 Kylian Mbappe baada ya kukosa kumsajili mchezaji mwenza raia wa Brazil Neymar, 27. (Mundo Deportivo - in Spanish)
West Ham iliipiku Bayern Munich ili kuweza kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 Sebastien Haller kutoka Eintracht Frankfurt msimu huu katika usajili utakaovunja rekodi wa £45m. (Mail)
Watford ilimfuta kazi mkufunzi wake kwa kuwa hakuweza kuimarisha safu ya ulinzi na alikuwa hataki kuwachezesha baadhi ya wachezaji wapya waliosajiliwa.. (Sky Sports).
Nafasi ya kipa wa Manchester United David de Gea inaweza kupewa kipa mlinda lango mwengine ili kujaza pengo hilo huku mazungumzo kuhsu kandarasi ya mchezaji huyo yakiendelea. (Marca - in Spanish)
David De Gea
De Gea, 28, ameripotiwa kutia saini kandarasi ya miaka mitano katika uwanja wa Old Trafford. (Record)
Beki wa Ubelgiji Jan Vertonghen, 32, anataka kutia kandarasi mpya na klabu ya Tottenham huku mkataba wake ukitarajiwa kukamilika mwisho wa msimu huu. (Football Insider)
Spurs pia wamempatia kiungo wa kati Christian Eriksen kandarasi mpya ya £230,000 kwa wiki ili kujaribu kumzuia huku klabu za Man United na ile ya Real Madrid zikimnyatia.. (Mail)
Christina EriksenHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Southampton ina hamu ya kumsaini kinda wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 18 Yari Verschaeren kutoka Anderlecht. (Calciomercato - in Italian)
Beki wa Cardiff na Ivory Coast Sol Bamba, 34, ni miongonii mwa wachezaji wanaotarajiwa kumrithi Neil Warnock atakapojiuzulu kama mkufunzi mwaka ujao. (South Wales Evening Post)
Manchester City na Manchester United zinamnyatia kiungo wakati wa Benfica kinda Florentino Luis, 20. (Mirror)
Florentino Louis
Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce anasema kwamba alijaribu kumsaini beki wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk, 28, akiwa mkufunzi wa Hull. (Guardian)
Jose Mourinho anasema kuwa mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard ana kila uwezo wa kuwa mmojawapo wa wakufunzi bora katika klabu hiyo ya Stamford Bridge. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa Tottenham na Ireland wa timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Troy Parrott, 17, analengwa na Juventus Juventus, Real Madrid Bayern Munich. (Calciomercato - in Italian)
Wlfried Zaha
Mino Raiola ni miongoni mwa baadhi ya maajenti wanaotaka kumwakilisha mshambuliaji wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoa notisi ya lengo lake la kutaka kuiwacha kampuni inayomsimamiaUSM. (Mail)
Valencia na Benfica zina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Crystal Palace na England Jadan Raymond, ambaye bado hajatia saini ya kushiriki mechi za kulipwa katika uwanja wa Selhurst Park. (Mail)

Post a Comment

0 Comments